Naye Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili Tanzania Christina Shusho, anatarajiwa kufyatua burudani kwenye tamasha la kimataifa la kuipenda Tanzania litakalowika ndani ya Viwanja vya Jangwani kuanzia Agosti 11-12 mwaka huu.
Kwani Tamasha hilo litakuwa ni laaina yake huku likipambwa na michezo mbalimbali, ikiwamo ya sarakasi na waendesha pikipiki na baisheli wa kimataifa watakaokuwa wakizirusha hewani.
Alisema kutakuwa na jukwaa la pekee la watoto watakaoburudishwa na msanii maalum, kutoka nchini Uingereza hivyo wanafamilia wanakaribishwa waje na watoto wao ili waburudike.
Tamasha hilo ambalo litaongozwa na Mwinjilisti wa Kimataifa, Andrew Palau, limelenga kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru kwa lengo ni kuonyesha upendo ambao Mungu amelionyeshea taifa hili.
Alisema pia kutakuwa na timu ya watu kutoka mataifa mbalimbali ambao wamekuja kujitolea kwa kushirikiana na makanisa katika kutoa huduma za kijamii.
Tamasha hilo litafanyika Jumamosi na Jumapili kuanzia saa 7:00 mchana hadi jioni.
No comments:
Post a Comment