Tuesday, August 7, 2012

MAISHA YA WOKOVU YAMEKUWA KAMA MTINDO KWA ULIMWENGU WA SASA


Inasikitisha sana kuwa kwa sasa watu wengi wamefanya maisha ya wokovu kama mtindo na dhambi ni kitu cha kawaida kwao, kwani imefika kipindi wanatafuta maneno mazuri ya kuipamba dhambi ili ionekane kuwa ni kitu cha kawaida.

Na zaidi ya yote wanafanya jitihada kuonekana mbele za watu, kuwa ni wema na hawafanyi juhudi kukubalika mbele za Mungu.

Kitu cha msingi ambacho kwa mtazamo tu nimeng'amua ni kuwa tunaishi bila maombi... ndugu zangu ni ngumu kumshinda shetani bila maombi na kusoma neno kwani yatupasa tujitahidi kuwa na juhudi katika maombi ili kumlingana Bwana na kumshinda adui.

Kwani maisha ya maigizo ni hasara kwetu sisi na itakuwa huzuni kubwa tumepata neema ya kumjua Mungu na tukashindwa kuitumia, tusiishi huku tukimsulubisha Mwana wa Mungu kwa mara ya pili. Mungu atubariki sote na tutimize wokovu wetu kwa hofu na kutetemeka....by Deo Meck

No comments:

Post a Comment