Wakati Watu Wakiwa Kwenye Pilika Pilika za Christmas na Zikiwa Zimebaki siku 13 kwa Msaada wa Mungu tumalize Mwaka 2012 na kuingia mwaka mpya wa 2013 kila mtu ana jambo la kuuongelea mwaka huu ambao unamalizika malizika. Ni Mengi yamepita mwaka 2012 na Mengine yakuchekesha na mengine ya kuliza lakini ndio mwaka unamalizika.
Tunapoelekea
mwaka 2013 kuna baadhi ya Makampuni yamesha andaa viapaumbele vyao kwa
ajili ya mwaka unaofuata, Kuna Familia kama Familia zimekaa na kupanga
mipango yao kwa ajili ya Mwaka unaofuata na kuna watu binafsi ambao wao
wamasha evaluate kwa mwaka 2012 na kuandaa mipango mbalimbali kwa ajili
ya mwaka 2013.
Kwa
utamaduni wetu wa Kitanzania tumejifunza kuwa kukosea ni kitu kibaya
sana na tunatumia muda mwingi kujipanga tusikosee na inapotokea
tumekosea hali tunayojisikia haitupi tena changamoto ya kujaribu tena
jambo ila zaidi ya kuliogopa. Kama mtu aliwahi jaribu biashara mwaka
2012 halafu akapata hasara kinachotokea ni mtu huyo kuto kutaka kabisa
kusikia kitu kinachoitwa Biashara kwenye maisha yake. Kama mtu aliingia
kwenye mahusiano na mwisho wa siku kupitia mahusiano hayo akaumizwa basi
kwenye ubongo wake na moyo wake anatokea kuchukia kitu kinachoitwa
mahusiano. Kama alipata hasara kwenye Kilimo basi chochote unachomwambia
kuhusu Kilimo kwake linageuka kuwa ni jambo la kulitazama mara mbili
ama mara tatu sababu tayari ana kumbukumbu mbaya na Suala zima la
Kilimo.
Kujitathimini
na Kusahihisha kupitia makosa tunayoyafanya kwenye maisha ni jambo
lenye kuleta maendeleo kwa kila mtu mwenye nia ya kuendelea mbele.
Wahenga walisema tunajifunza kutokana na makosa. Kwenye Biblia ukisoma
kuna story maarufu sana ya Mtu anaitwa "Mwana Mpotevu" yamkini hili iso
jina lake halisia inawezekana anaitwa James, Anna, Rose ama hata
Filikunjombe lakini kwa kumbukumbu njema akaitwa kwa sifa yake "Mwana
Mpotevu" ukisoma vizuri huyu Kijana hakuwa amepotea alienda mahali kula
bata wa kutosha baada ya kupata urithi. Yamkini Mwana Mpotevu hana
tofauti sana na wengi wetu katika Maisha Chanzo cha fedha cha Mwana
Mpotevu ni Urithi, yawezekana wewe Chanzo Cha Fedha ni Mshahara, ama
Biashara matumizi ya kutapanya kama yale ya Mwana Mpotevu kila mtu
anayo, Mwana Mpotevu angekuwa na Option ya kukopa kama wewe pengine
angekopa, Mwana Mpotevu angekuwa na Option ya Mpesa angeomba kwa rafiki
zake, tofauti ni kwamba wewe unaishi kwa madeni Mwana Mpotevu hakuwa na
Option hata moja zaidi ya kula Chakula Cha Nguruwe. Tofauti inakuja
kwenye Kuji Evaluate na Kuchukua hatua za mabadiliko Chanya. Wengi wetu
tuna jitathimini lakini tunarudia makosa yale yale tunayoyafanya kila
iitwapo leo. Hatua madhubuti za mabadiliko zimekuwa kwenye makaratasi na
mioyoni lakini sio katika matendo.
Kubadilika
kunahitaji discipline hasa unapoamua kubadilika kwa kuacha kitu
unachokipenda, yamkini katika tathimini utabaini kuwa Usingizi na Kulala
kusiko na sababu ndiko hasa kumesababisha uwe hivyo ulivyo sasa
unapoamua kubadilika kuacha kulala kitu unachokipenda ni changamoto
inayohitaji nidhamu. Yamkini utagundua asilimia kubwa ya matumizi ya
fedha zako ni starehe, mavazi na anasa na umejikuta umekuwa haufanyi
akiba ya fedha zako, usitegemee kabisa ukiamua kubadilika mambo yatakuwa
rahisi kama unavyodhani inahitaji nidhamu.
Kuna
makosa mengi sana yamkini tumefanya mwaka 2012 mengine kwa kutambua na
mengine pasipo kutambua lakini mwisho wa siku matokeo yake hayakuwa ya
kupendeza na kufurahisha, jitathimini kwa kina kwanini ulianguka,
Usitazame tu wapi umeangukia bila kutazama kwanini ulianguka bila shaka
itapekelekea wewe kuanguka tena na tena kwenye maisha. Kwanini usikae
mahali ukajifungia ukatathimini mwaka 2012 ulikopita ukayatazama mazuri
uliyoyafanya na kuongeza tija katika yale mazuri na ukayatathimini
changamoto ulizokutana nazo mwaka 2012 na kuona ni namna gani
ulichangamotika ili changamoto hizo uweze kuhitimu mwaka 2013. Ni
Kujidanganya kuingia mwaka mpya bila kujua wapi unakwenda na nini
unataka kufanya Kimaisha. Kurudia mambo yale yale na namna ile ile ya
kufanya itasababisha tusipige hatua kwenye maisha yetu ya kila siku.
Hatuwezi tukawa tunaishi kama wanyama wasio na akili wanaoishi kila siku
bila kujua nini kinaendelea kwenye maisha yao. Kwa kadri miaka
inavyokwenda ndivyo tunavyokaribia uzee na changamoto zake mwisho wa
siku mambo miaka 10 ijayo tutajilaumu sana kwa mambo ambayo
hatukuyafanya leo.
Bado
unayo nafasi ya kujitathimini upya, jipange sawa sawa kukabiliana na
changamoto za mwaka 2013 itakuwa ni ajabu jambo lile lile ulilochemsha
mwaka 2012 ukachemsha mwaka 2013 kwa namna ile ile.
Think Differently and Make a Difference.
By
Papaa Ze Blogger.
0713 494110