Thursday, September 13, 2012

Udhihirisho Wa Nguvu Za Mungu Wafunika Hema Ya VCCT

 Semina ya Neno La Mungu Inayofundishwa na Pastor Adam Haji Katika kanisa la VCCT chini ya Dr. Huruma Nkone imeambatana na Udhihirisha wa Nguvu za Mungu tangu siku Ya Jumapili ilipoanza.

Semina hiyo yenye mafundisho ya neno pamoja na huduma ya Deliverance imewafungua watu wengi waliofungwa na nguvu za giza na kuwaacha huru baada ya kukutana na nguvu za Roho Mtakatifu ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.

Ikiwa leo ni Siku ya 6 ya Semina ambapo semina hufanyika katika Hema Ya VCCT iliyo Mbezi Beach Kawe Kuanzia Saa 11 jioni Mpaka saa 2 Usiku katika hema hiyo. Huduma ya Neno la Maarifa na Uponyaji hufanyika Katika hema hiyo.

Kwa Mawasiliano zaidi ukitaka kufika katika Semina Wasiliana na namba hiyo hapo 0713 494110.




 Pastor Adam Haji akiwa na Dr. Huruma Nkone Katika Huduma Ya Maombezi siku ya Juzi
Add caption

 Watu wakishangaa mara baada ya kuamrishwa kuvua heleni hizi mara baada ya Kuvua she was completely delivered

 Nguvu Za Mungu Zikiwa Kazini siku Ya Jana

 Hapa Ilikuwa Juzi Kwenye Semina.

 Mbele za Uwepo.

 Adam Haji akiwa Kikazi Zaidi siku Ya Jana.

Chris Mauki na Miriam Lukindo wa Mauki Wakiwa Makini Katika Semina.

HApa alikuwa akifundisha namna ya Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu wanavyofanya kazi ndani Ya Mwamini na ambayo Lucifer, Majini na Mapepo Yanavyo Copy na Ku-paste utandaji kazi wa Mungu.

Dr. Nkone akiwa Kikazi Zaidi siku Ya Jana.

Pamoja na Tiba za Hosipital Kumbe huyu Mtoto alikuwa akiteswa na nguvu za giza.

Somo la Juzi lilikuwa tamu zaidi ambapo alikuwa akifundisha ni namna gani ndoa nyingi siku hizi zimekuwa na migogoro kumbe wanandoa wengi wanaingia kwenye ndoa huku wakiwa na "Covenants" na mahusiano yao ya siku za nyuma.

Mdada akishangaa Pete ambayo alikuwa ameivaa iliyokuwa inatumiwa kama Point Of Contact katika Ulimwengu wa roho wa mapepo. Siku Ya Jana Mdada huyu aliwafanyiwa deliverance kutoka katika kifungo. Pete hiyo alikuwa amepewa na ndugu yake ambaye alimfunga asifanikiwe katika maisha.

Hapa akionesha mtu ambaye anaingia kwenye ndoa huku alikuwa na mahusiano shule, ofisini, mtaani then huyu Mtu anaamua kuoa Mke Mmoja huku akisahau kuwa kuna agano katika Kila tendo la Sex...Jiulize TUKO WANGAPI??

 Parking Full.

 The Other Side Of parking.

Pastor Adam Haji akiwa amemvua Pete iliyokuwa ikifanyika kama Point Of Contact ya Ulimwengu wa giza. Watu wakishangaa.

Dr. Huruma Nkone akimasaidia Mdada kusimama baada ya Maombezi siku ya jana.

Adam Haji akiongea na Mmoja wa Waliofunguliwa siku ya Jana ambaye alikuwa akivaa helen ambazo zilikuwa Point Of Contact katika Ulimwengu wa giza.

Huyu Mdada alipigwa na Butwaa baada ya Kuombewa na ufahamu wake kurejea akishangaa amefikaje Kanisani.

Ukitazama Vizuri huyu dada anaonekana akiwa na heleni zake wakati maombi yanaanza. Kwa Muda Mrefu huyu Mdada amekuwa akiteswa na nguvu za giza bila kufahamu kuwa hereni zake ndizo zilizokuwa lango la Ibilisi.

MAMBO AMBAYO WANAUME HAWAPENDI KUTOKA KWA WENZI WAO!!

1.Wanaume hawapendi kuambiwa cha kufanya na wenzi wao.
Mwanamke unapotaka mwanaume afanye jambo usimwambie alifanye bali fanya kama una mpa ushauri, kwamba John hivi kwa nini tusiweke Balbu hapa kwenye Korido maana kuna giza kweli.

Badala ya hivi wewe John huoni hapa kwenye korido kuna giza balbu imeungua mwezi sasa hujabadilisha kwa nini?weka balbu bwana.Atafanya au asifanye kabisa kwa sababu umemwambia cha kufanya.

2.Wanaume hawapendi mwenzi mwenye makelele,mlalamishi.
Yeye ni kulalamika kuanzia jumatatu hadi jumapili, japo wanawake nao wanasema kuna wanaume walalamishii balaaa.Na wenye gubu wanasusa kula mpaka kuongea wanawanunia wake zao mmmmh!

3.Wanaume hawapendi mwenzi mchafu.
Mchafu wa mwili wake na hata nyumbani kwenye suala la kutunza nyumba wanayoishi, na uchafu hufanya mwanamke apoteze mvuto.

4.Wanaume hawapendi mwenzi mbishi.
Japo na wanawake wanasema wanaume ndio wabishi zaidi.Utampa mwanaume ushauri lakini haufanyii kazi ubishi mwingi.

5.Wanaume hawapendi kuamrishwa na mwenzi wao.
Mwenzi mbabe anaetoa amri na kumtawala hawataki.

6.Wanaume hawapendi kuhisiwa hisiwa na kusachiwa sachiwa.
Kumpekua kwenye simu,mifuko ya suruali kwamba unamulika mwizi na hawapendi tena pengine hawajafanya jambo la kuwafanya wahisiwe vibaya.

Hizi ni baadhi tu japo kuna vitu pia wanawake hawavipendi kutoka kwa wenzi wao wanaume.
.......Thank You Dina Marios

Madaktari nchini Kenya waanza Mgomo

Madaktari nchini Kenya leo wanaanza mgomo wao kushinikiza nyongeza ya mishahara huku sekta ya afya ikiwa katika tisho la kuathirika.

Madaktari hao watajiunga na Walimu na wahadhiri wa vyuo vikuu ambao wamekuwa wakiendelea na migomo kwa wiki ya pili sasa.

Madaktari hao kutoka hospitali za umma wanasema kuwa serikali imepuuza onyo lao la kugoma ikiwa haitatimiza matakwa yao.


Madkatari wa Kenya katika maandamano ya mgomo

 Madaktari hao wanasema kuwa serikali iliwahadaa baada ya kukataa kutekeleza makubaliano waliyoafikia mwezi Disemba mwaka jana ya kutimiza matakwa yao ya mishahara bora na mazingira mazuri ya kazi na mafunzo ya kitaaluma.

Mariam Dodo Abdallah amezungumza na Daktari Victor Ng'ani, ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Madaktari hao wanaogoma, na kwanza kumuuliza kilio chao hasa ni kipi ?..Kutoka BCC Swahili

Monday, September 10, 2012

MATUKIO MBALIMBALI KWENYE IBADA YA J'PILI NDANI YA KANISA LA VCCT m


Mch. Adam Hajj Mohamed akimsifu Mungu



Mch. Joyce Nkone kulia akiwa na ubavu wa Mch. Haji

Mch. Adam Hajj Mohamed na Mch. Huruma Nkone wakimsifu Mungu




Mch. Adam Hajj Mohamed akiwa na mkewe kabla ya kuanza mafuindisho ya Semina

Vijana wa VCCT wakimleta mratajiwa (Bwana hARUSI Mtarajiwa) huku wakiwa mawembeba juu

Bwana Harusi mtarajiwa ndani ya suti

Watarajiwa hao wakielekezwa cha kufanya na Mch. Huruma pindi walivyotangaza nia siku ya jumapili ndani ya VCCT



Mch. Huruma Nkone akiibariki pete ya wachumba hao waliotanganza nia jana

Tendo likifanyika..safi sana wapendwa

Mtarajiwa akiwa anatamka maneno aliyokuwa akitamka Mch. Huruma Nkone


Baba na Mwana

Safi sana vijana wa VCCT




Nikiwa na Mtumishi Mussa








5Pipo ndani ya Pozi