Thursday, August 2, 2012

Love Tanzania Festival yabisha hodi



Huwa ni Tamasha la Kihistoria Barani Afrika, kwani tamasha hilo la kiinjili limewahi kurindima  ndani ya majiji kadhaa barani Afrika.

Si lingine bali ni lile Tamasha la Love Tanzania Festival, linatarajia kuwika hapa Jijini kuanzia Agosti 11-12 mwaka huu ndani ya Viwanja vya Jangwani.

Makanisa zaidi ya 800 yatajumuika kwa pamoja, wakiwemo na watu wa madhehebu mbalimbali ndani ya viwanja vya Jangwani.

Tamasha hilo la Love Tanzania Festival, lipo chini ya Andrew Palau kwani atawasilisha ujumbe wa Upendo kwa watanzania..ni tamasha la kabambe na siyo la kukosa.

Na tukio hilo la kipekee litashirikiana na Shirika la Luis Palau la nchini Portlan/Marekani, huku likijumuishwa na makanisa yapatayo mia nane na zaidi ya madhehebu mia mbili ni washiriki.

Mbali na hayo kutakuwa na mabmo mbalimbali kwenye tamasha hilo ni pamoja na miwani 10,000 za kusomea zitatolewa bure,.......

Naye mmoja wa waandaaji wa tamasha hilo kwa hapa jijini Prosper Mwakitalima, alisema kwamba lengo la tamasha hilo la kuwakutanisha watu wa Dini, Makabila mbalimbali na rika zote ni kumtukuza Yesu Kristo.

Mwakitalima alisema kwamba kabla ya shughuli ya tarehe 11-12, kutakuwa na mambo mbalimbali ambayo Love Tanzania Festival itakuwa ikiifanyia jamii ya Tanzania.

Mambo hayo ni pamoja na Mbeba maono wa Love Tanzania Festival Mtumishi Andrew Palau, atahubiri ibada  zote mbili ndani ya kanisa la Upanga City Christian Centre (VCC) ambalo itakuwa ni siku ya Agosti 5 kuanzia mishale ya saa 7:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni.

Agosti 7 Andrew Palau pamoja na wachungaji,Maaskofu, Waimbaji kikiwemo na kikundi cha wanamichezo ya Baiskeli, watakuwa wakilonga nawaandishi wa habari mbalimbali ndani ya Ukumbi wa TBD.

Mishale ya saa 11:30 jioni ya Agosti 7 ndani ya Ukumbi wa Karimjee, kutakuwa na WOMENS DINNER ambapo zaidi ya wamama 600 siku hiyo watapata nafasi ya kumsikiliza Andrew Palau huku wakibadilishana naye mawazo.

Agosti 8 ndani ya Ukumbi wa Karimjee Hall kuanzia saa 12:00 jioni kutafanyika halfa ya chakula cha jioni, viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo na wafanyabiashara wakubwa watapata nafasi ya kukutana na Palau, ambapo mtumishi huyo atatumia nafasi hiyo kumtangaza Kristo kwa mkusanyiko huo wa Watanzania.

Mbali na hilo Agosti 8 kuanzia saa 8:00-9:00 jioni kutakuwa na mazoezi (Rehesal), ya michezo ya Baiskeli ambapo kikundi cha JUNGLE RUSH FMX kutoka Afrika ya Kusiki kitafanya mazoezi hayo kwa dhumuni la kujiweka sawa.

Baada ya mazoezi hayo kutakauwa na maombi kwa ajili ya kuuombea Uwanja wa Jangwani, kwa shughuli nzima itakayofanyika Agosti 11-12 mwaka huu viwanjani hapo.

Tamasha hilo la Love Tanzania Festival mabli na kuhusisha masuala ya uponyaji wa Roho za watu kupitia neno la Mungu, kutakuwa na madaktari maalumu wa macho kutoka nchini Marekani huku wakishirikiana na Madaktari wa hapa nchini Tanzania watakuwa wakipima bure watu mbalimbali wenye matatizo ya macho.

Hata wale wenye matatizo ya kutoona vizuri maandishi watapewa Miwani za kusomea bure, na jumla ya miwani zipatazo elfu kumi zitatolewa kwa ajili ya wale watatakao bainika kwamba wanamatatizo ya macho.

Ratiba ya Kliniki hiyo itakayokuwa na vituo vinne ni pamoja na :

Kituo 1:St.Nicholaus Anglicana Church-(Ilala)

Kituo cha 2:Tanzania Assemblies of God-(TAG-Mbagala)

Kituo cha 3:Lutheran Church-(Vingunguti)

Kituo cha 4:Baptist Mission Church-(Magomeni)

Kliniki zote zitaanza kuanzia asabuhi ya saa nne, mpaka saa kumi jioni.








No comments:

Post a Comment