Si mwingine bali ni yule mwimbaji wa muziki wa Injili hapa nchini, Miriam Lukindo Mauki ‘Binti Afrika’ anatarajia Jumamosi hii anatarajiwa kuiteka Matembele ya Pili, Ukonga jhapa Jijini kwenye uzinduzi wa albamu mbili za kwaya ya Sauti za Sifa iliyo chini ya Huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM).
Naye Mwalimu wa kwaya hiyo, Elibariki Isango, alisema, Miriam amekubali kuja kuwaunga mkono kwenye shughuli yao ya kuzindua albamu zao mbili kwa kuimba nyimbo mbalimbali.
Alisema kwamba lengo la uzinduzi wa albamu hizo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la huduma hiyo, ambalo kwa sasa lipo kwenye hatua za mwisho.
Na kila atakayefika katika uzinduzi huo na kununua CD zao, atakuwa ametoa sadaka yake ya kukamilisha hekalu la Bwana.
Waimbaji wengine watakaoimba kwenye uzinduzi huo ni pamoja na Ami Mwakitalu, Madame Luti & Chris, Faraja Moleli, Queen Talaba, Wilson John, Magreth na wengine wengi, ambako shughuli itaanza majira ya saa 6:00 mchana na kumalizika saa 12 jioni.
Mbali na hilo kwenye uzinduzi huo hakutakuwa na kiingilio, wadau wa muziki wa Injili wameombw akumiminika kwa wingi siku hiyo ya Jumamosi hasa wale wakazi wa Kitunda, Ukonga na hata Gongolamboto.
Mama Lukindo akiwa akilitawala jukwaa katika moja ya kazi zake |
No comments:
Post a Comment