|
Obedy |
|
The voice wote kwa pamoja wakiwa na Jimmy Temu |
|
Josia na Baraka wakiteta jambo fulani huku Josia akiandikamwaga wino.
|
| |
The Voice katika packing ya Praise power Radio | |
|
Josia Sadoki(Mzee wa bass) akitabasamu akiwa ndani ya gari. |
|
The voice wakipokewa na uncle Jimmy katika viunga vya PPR |
|
Baada ya kumaliza kilichowaleta sasa wanaondoka kwenda mazoezini |
Obedy John Mark anazidi kumshukuru Mungu kwa kumponya ajali mbaya iliyotokea hapo awali, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu aliweza kunusurika kwenye kwa kugongwa na kwneda kuangukia mtaroni.
Kwani alipata ajali akiwa ndani ya Bajaji maeneo ya Sinza akielekea Magomeni, akiwa na dereva wa bajaji waligongwa na kutumbukia mtaroni na kuumia uti wa mgongo pamoja na mbavu na kukimbizwa hospitalini.
Baada ya muda mfupi watu mbalimbali wenye mapenzi na kundi hilo la The Voice, walikwenda kumfariji na kumpa mkono wa pole mwimbaji huyo wa kundi la The Voice.
Mungu ni mwema asikwambie mtu..jamani kwa Yesu kuna raha ya ajabu, umuombe nini asikupe, ukimtafuta anapatikana, ukibisha anafungua, ukimuomba anakupatia yale umuombayo kwnai mkono wake si mfupi ushindwe kukufikia, yeye si kipofu asindwe kuona yale uyapitiayo kwneye maisha yako ya kila siku, yeye si kiziwi ashindwe kusikia kilio chako...Mungu ameweza kusikia sala za vijana hawa juu ya mwimbaji mwenzao Obedy kuweza kupona.
Baada ya uponyaji huo kwa Obedy aliweza kuambatanana wenzake wa The Voice kumshukuru Mungu na kuwashukuru watu wote waliojitokeza, kwenda kumfariji pindi alipopata ajali kwani shukrani hizo zilikuwa ndani ya Praise Power Radio.Shukrani nyingine alizipelekwa kwa uongozi wa PPR, kwa uzalendo wao kwa kuwaunganisha kwa watu kujitokeza kumwona huku wakimfariji pindi alivyokuwa amelazwa hospitali.
No comments:
Post a Comment