Mwanamuziki huyo ataimba vibao vyake vyote kwenye Uzinduzi wa albamu ya pili, ya kwaya hiyo ndani ya Ukumbi wa WRM.
Si mwingine bali ni yule mwimbaji wa nyimbo za kumtukuza Mungu Christina Shusho, anatarajia kulitawala jukwaa moja na kwaya ya nyimbo za kusifu na kuabudu iitwayo Sauti za Sifa ya Huduma ya ‘The Word of Reconciliation Ministries’ (WRM) iliyopo Matembele ya Pili Kivule, hapa Jijini Agosti 25 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwalimu wa kwaya hiyo, Elibariki Isango, alisema Shusho ataimba vibao vyake vyote katika uzinduzi wa albamu mbili za kwaya hiyo ndani ya Ukumbi wa WRM.
Siku ya uzinduzi wa albamu hizo ‘Heshima na Utukufu’ na ‘Enendeni kwa Roho,’ Shusho naye atakuwepo huku akiimba nyimbo zake zote zilizomtambulisha katika muziki huo.
Mbali na Shusho kulitawala jukwaa waimbaji wegine wa muziki huo kutoka hapa Jijini na Arusha watalitawala jukwaa siku hiyo.
Na fedha zitakazopatikana kwenye uzinduzi huo, zitatumika kumalizia ujenzi wa jengo la huduma hiyo, ambalo lipo katika hatua za mwisho za kukamilika.
No comments:
Post a Comment