Mbali na hilo watu wengi watu wengi siku hizi wamekuwa wakiishi maisha ya ndoa kama fasheni hali ambayo imekuwa ikishusha hadhi ya ndoa, na si jambo la ajabu kusikia ndoa iliyofungwa wiki moja iliyopita imevunjika baada ya wanandani hao kutwangana makonde na kusambaratika.
UNAFAHAMU KWAMBA KATIKA NDOA KUNA MATABAKA MAKUU MAWILI?
Tabaka lwa kwanza ni kwa wanandoa kufurahia Ndoa yao na tabaka la pili ni la wanandoa kuijutia ndoa yao, hakika ndoa inaraha sana na nitendo la heshima mbele za Mungu.
Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini siku ya Harusi wanandoa wote huwa na furaha? Na Je? furaha hiyo baadaye hupotelea wapi? Hakuna mwanandoa yeyote ambaye huwaza kama siku moja yeye na mwenzi wake wanaweza kukorofishana na kutukanana matuzi mazito ambayo hugeuka kuwa sumu ndani ya ndoa yao.
Siku ya harusi kila mmoja huisubiri kwa shauku kubwa na kuona siku kama haziendi ili wanandoa hao wawe pamoja kwenye jahazi la ndoa ya maisha. Baada ya muda mambo hubadilika kwa baadhi ya wanandoa pindi wanapoanza maisha ya pamoja.
Kabla sijaendelea naomba kukuuliza wewe uliyendani ya NDOA...Je ulishawahi kujiuliza ni kwanini furaha mliyokuwa nayo wakati hamjaoana leo hii haipo tena? Kumbuka mara nyingi penzi linalotolewa wakati wa uchumba huwa lina mbinu nyingi za kusomana tabia na kila mmoja hupenda kuficha tambia yake mbaya aliyonayo.
Ni suala gumu kigodo kwa wanandoa ambao kila mmoja amekulia kwenye malezi tofauti kukaa na kujenga tabia moja. Wakati watu wanapokuwa katika hatua ya uchumba hushindwa kusomana vizuri tabia zao ni kutokana na umbali walionao.
Kwa sababu kila mmoja anakuwa kwao ama kwake hali ambayo hutoa muda mwingi wa kumkumbuka mpenzi wake.( Ama hakika ndoa ni furaha, Kabla ya kutamka maneno ya ahadi mbele ya mashahidi kanisani huku taaaratibu wakivishana Pete ya Ndoa mme wake mpendwa fulani tayari kwa kuanza safari ya maisha ya ndoa yeye raha teeeeele!) Kipindi hicho wachumba hao hutumiana ujumbe mfupi kupitia mitandao kama Simu ama Email ili kila mmoja kuonyesha ni kwa jinsi gani anampenda mwanandani wake mtarajiwa.
Wahusika hao hujitahidi kutumiana maneno mazuri na yenye kuvutia hisia ya mahaba hali ambayo uzidi kuongeza upendo kwa pande zote mbili, na maneno hayo huongeza shauku kwa walengwa hao kuwa na shauku ya kuwa pamoja wakidhani kuwa siku zote mambo yatakuwa hivyo.
Kwa kipindi hicho wachumba hao huwa wanaelewana kwa kila jambo wanalopenda lifanyike na furaha ya Uchumba huo kama nilivyosema hapo awali hunogeshwa na umbali uliopo kati ya wahusika hao.
Wakati mwingi mmoja wapo anapotakiwa na mwenzake wakutane sehumu wanayoona inafaa kwa ajili ya mazungumzo yao ya faragha, na hulazimika kuwadanganya wazazi wao ama ndugu zao wanaoishi nao kwamba wanaenda kwa jamaa zao na atachelewa kurudi.
Pindi mazungumzo yao yanapoanza huku muda ukizidi kwenda wachumba hao hutamani muda urudi nyuma ili waendelee kuongea na kupeana habari za hapa na pale kuhusu maisha yao ya badae, sasa shauku hiyo ya kuwa pamoja hupotelea wapi baada ya kuoana ambapo huwa kuna muda mrefu wa kuwa pamoja tofauti na kipindi kile walipokuwa wanaona muda unaenda na mazungumzo yao bado yanaendelea?
Nadhani utaungana na mimi kwamba kwa baadhi ya wanandoa mambo hayo hupotea pindi wanapoingia ndani ya ndoa kutokana na muda mwingi kuwa pamoja, na utakuta wanaongea mambo yao mpaka yanaisha.
Siku zote mwanadamu hakosi kuwa na madhaifu maishani mwake, kipindi hicho wanandoa hujikuta wapo kwenye wakati Mgumu pindi mmoja wapo anapofanya kosa hata si kwa makusudi.
Na inawezekana akawa ni mama kawa mkorofi ama baba ama wote kwa pamoja, na hiyo humfanya kila mmoja kujiona anahaki ya kufanya atakavyo na hayupo tayari kukosolewa.
Ni imani yangu kuwa kila mwanandoa siku ya kufunga ndoa huwa kunaviapo ambavyo hutamkwa na wahusika wote, kwamba watakuwa tayari kuishi kwenye maisha ya raha na shida, iwe magonjwa nk. Lakini mambo huwa sivyo pindi safari ya maisha ya NDOA inapoanza.
SUMU YA MAISHA YA NDOA
Hakuna asiyefahamu kwamba asilimia kubwa ya vitu tunavyovitumia vina sumu, na hatuoni madhara ya sumu hiyo kutokana na kufuata taratibu za matumizi na vitu tunavyovitumia. Kwa Mfano mzuri ni dawa ya panado ambayo mtu anapoumwa kichwa hutumia dawa hiyo ili kuondoa maumivu hayo, na dawa hiyo huwa haitoi madhara yoyote. Lakini dawa hiyo ukinywa kinyume na masharti yake lazima madhara uyapate kama si kufa tambua utaugua zaidi.
Mambo hao kwanza kabisa ni heshima, upendo wa dhati, mawasiliano mazuri katika familia, kusaidiana na Uvumilivu. Haya ni mambo muhimu sana kwa wanandoa.
Kumbuka kwamba wanandoa wanaokosa mambo kama Heshima, Upendo wa dhati, Mawasiliano mazuri kwenye familia ndoa yao lazima iwe mashakani na ugomvi hauwezi kuisha kamwe. Kwa wanandoa upendo unapotawala ndani ya nyumba huifanya ndoa hiyo kuchanua kila mara na hiyo huambatana na uvumilivu.
Neno jingine ambalo wengi huliona kama halina maana ni SAMAHANI... pindi mmoja wenu anapokosea, inapotokea ukamkosea mwenzako jitahidi kuomba samahani badala ya kukaa kimya na ukifanya hivyo itaonekana unadharahu ana kiburi.
Ukiyazingatia hayo yote ni lazima ndoa yako iwe na furaha siku zote. Kwa leo niishie hapa baada ya hapa nitakulete sababu za mwanamke kwenda nje ya ndoa, na kisha mwanaume naye kwenda nje ya ndoa. Nakaribisha maoni na ushauri juu ya yale uliyoyasoma hapo juu. Pia na wewe unaruhusiwa kutoa somo ama kufundisha jambo lolote ulilonalo kwa ajili ya faida ya sisi tusiojua....Je Sababu hizo za wanandoa kutoka nje ya Ndoa wazijua ni zipi?....Ambatana nami wiki ijayo siku kama ya leo.
No comments:
Post a Comment