Saturday, September 1, 2012

VIJANA WA KILEO NA MAHUSIANO

Kwani wengi wao hujaribu kufuata kanuni au shuhuda za watu kuhusu wao walivyofanya, ili kupata wake/waume zao badala ya Kuangalia kile ambacho neno la Mungu linasema kuhusu jambo hilo.

Kama ni kijana kama mimi na unapenda kufanikiwa katika maisha yako ya mahusiano na hatimaye ndoa ili uwe baba/mama wa kuigwa na kila mtu ni lazima ujue na kuzizingatia kweli hizi mbili kuhusu Mahusiano ya watu hawa wa Imani.
 
ISAKA NA REBEKA

Biblia inasema muda wa Isaka kuwa na mke ulipofika, Mzee Ibrahimu alimwita mmoja wa Wafanyakazi wake na akamwambia maneno yafuatayo; "Enenda katika nchi yangu na jamaa zangu, na umtwalie Mwanangu Isaya Mke toka huko... na si miongoni mwa hawa Mabinti Wakaanani"

Na kwa kusisitiza hilo, Biblia inasema alimlisha kiapo mbele za Bwana, ili kuhakikisha ya kwamba haokotezi Mwanamke yeyote pale na kumletea Isaka.

Unajua ni Kwanini Ibrahimu aliamua kufanya hivyo?

Ni kwa sababu alishajua ya kwamba Yeye na familia yao ni watu maalumu[Wenye agano na Mungu] hawawezi kujichanganya na watu wasiomcha Mungu wao na wasioishi sawa na kanuni za Mungu aliye hai...

Vijana wengi wanajaribu hata kutafuta wasichana/wavulana nje ya makanisa, wanawaleta kanisani wiki kadhaa, au miezi kadhaa au mwaka...lengo sio kuwaleta kwa Yesu bali kuficha uovu wao na hila yao ya kuwa na mahusiano na watu wasio na Uhusiano na Yesu....Wanafanikiwa na hatimaye ndoa zinafungwa.

Kinachofuata hapo wote tunajua, wale watu wanarudi kwenye maisha yao ya dhambi na wanakuwa miiba kwa hao wadada/wakaka waliowaleta...ndoa si ndoa tena bali ndoana...Kisa, Upumbavu na kutoliheshimu NENO LA MUNGU!

Nendeni mkawataufute akina dada/kaka nje ya Kristo, wawaoe/waolewe na nyie, ila mtakapokuwa mnakipata cha moto msitusumbue kuja kuamua kesi zenu...Kama mmekubali Kuliasi neno la Mungu na Kanuni za Ufalme wa Mungu basi Mkubali kupata matokeo yake na Muwe teyari kupata na Mafao yenu.

Lakini pia katika Nyumba ya Bwana nako si Salama kwani si aliyeko Kanisani  Ameokoka, Ananena kwa Lugha,  Anatoa Pepo, Anampenda Yesu, Anafaa kuolewa/Kuoa yatupasa kuzingatia hili na si kila aliyekanisani hufaa kuwa Mmeo/Mkeo.

Ukisoma habari ya kupatikana kwa Rebeka kuwa mke wa Isaka utagundua kwamba katika ile nchi ya akina Ibrahimu [kwa sasa tunaweza kusema kanisani] kulikuwa na Mabinti wengi sana, tena yawezekana wengine warefu, wafupi, weupe, maji ya kunde, wembamba, wasomi, wa familia bora au za wastani nk...

Lakini yule mtumishi wa Ibrahimu alikuwa na Ufahamu, Hekima na Maarifa ya Mungu ambayo yalimsaidia kumpata mtu sahihi wa kuolewa na Isaka...Biblia inasema, "ALIMWOMBA MUNGU" na Mungu akamsaidia kupata mtu sahihi kati ya mabinti wengi wenye Vigezo waliokuja pale kisimani kuchota maji!

Vijana wengi hawana muda wa kuomba kwa Mungu ili awasaidie awape hekima na maarifa na roho ya ufahamu ili waweze kukutana na watu sahihi wa maisha yao...na wengi hutegemea kanuni na Elimu za dunia hii wanaangukia pua...Mungu akusaidie, Mungu ayafunguwe Macho yako wewe ambaye bado uko kwenye Boti ya Singles kama nilivyo mimi na wengine.

No comments:

Post a Comment