Wednesday, September 5, 2012

Kesi ya waumini wa dhidi ya Askofu Mokiwa yatupwa

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na waumini watatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK)  kumpinga Askofu Stanley Hotay, kuwa askofu wa Kanisa hilo.

Jaji Fatuma Massengi akitoa uamuzi jana, alisema mahakama hiyo imekubaliana na pingamizi zilizowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi, kuwa Mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa sababu kanisa lina katiba yake yenyewe na walipaswa kupeleka ngazi ya kanisa kabla ya kulifikisha mahakamani.

Alisema waumini hao wanapaswa kuzingatia katiba ya kanisa
hilo kwa kufuata taratibu ambapo suala la uchaguzi maamuzi ya mwisho yanafanywa ndani ya kanisa na siyo Mahakama.
Askofu Stanley Hotay

Kwa msingi huo, Jaji Massengi aliyatupilia mbali madai hayo bilaya kuwataka walalamikaji kulipa gharama za kesi.

Jaji akisema sababu nyingine ya kutupilia mbali kesi hiyo ni pamoja na wadai kudai kuwa namba SO4757 ni ya Bodi ya Udhamini wakati ni ya hati ya usajili wa kanisa.

Kesi hiyo ilifunguliwa na waumini watatu Lothi Oilevo, Frank Jacob na Godfrey Mhone ambao walikuwa wakiwasilishwa na wakili Menrad D'souza.

Mbali na Askofu Hotay, mlalamikiwa mwingine alikuwa ni Mkuu Kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu Dk. Valentino Mokiwa ambaye alimsimika
Askofu Hotay kuongoz DMK kunyume cha sheria na taratibu za kanisa.

Katika madai yao ya msingi, waumini hao walikuwa wanaiomba Mahakama imzuie Askofu Hotay kusimikwa kuongoza dayosisi hiyo, kwa madai kuwa uchaguzi ulikiuka katiba ya kanisa kwa madai kuwa askofu huyo alighushi vyeti.

No comments:

Post a Comment