Friday, September 28, 2012

KONGAMANO LA WANAWAKE.....MWEZESHE MWANAMKE KIUCHUMI KWA MAENDELEO YA FAMILIA

Jukumu la mwanamke katika familia ni muhimu sana kwanza....Wanawake walio wengi wanatamani kuwa na kipato cha kutosheleza malengo yao na ya Kifamilia.

Ujasiriamali unawawezesha Wanawake kufanikiwa kiuchumi, huku wakiendesha Familia na kufanya shughuli zao kwa mafanikio makubwa zaidi.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Bethel, Sheila Mumy Bethel
Kwani Kongamano hili limeandaliwa na Wanawake waliofanikiwa kiuchumi na wenye nia ya kusaidia Wanawake wengine waweze kufanikiw akiuchumi na Malengo ni Wanawake wote wenye ndoto za mafanikio.

Na moja ya mambo ya kijamii unayoweza kufanya kama mwanamke , ni kujitambua wenyewe kwamba wewe ni nani, nini unamaanisha na wapi unataka kwenda?

Kongamano hilo litaendeshwa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Bethel, Sheila Mumy Bethel litakalowika ndani ya Hoteli ya Holiday Septemba 30 mwaka huu kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 12 jioni na kiingilio ni Shilingi elfu 10,000 tu...Ukiwa kama Mwanamke unayehitaji ndoto zako zitimie na hujui ufanye nini...basi usikose kwenda kwenye Kongamano hilo kwani hautaondoka kama ulivyoingia hali utaondoka ukiwa na kitu tofauti na ulivyokwenda.

No comments:

Post a Comment