Sunday, October 28, 2012

Night of worship@CCC Upanga.

Night of Worship ni Event iliyokuwa ya namna yake katika Usiku wa jana ndani ya Kanisa la City Christian Center  (CCC) Upanga. Tamasha hilo lilikutanisha vikundi mbalimbali na watu kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam katika kulitukuza na kuliinua Jina la Yesu.

The Nextleve Praise and Worship Team ,CCC Worship Team ,VCC, Glorious Celebration, John Lisu,Pastor Safari na John Kagaruki na wengine wengi walikuwepo kuhudumu usiku huo.

Glorious Celebration walikuwa wanafanya Live Recording ya Album yao chini ya Kampuni ya Hackneel Video Production katika usiku wa jana ambapo ilikuwa ya baraka sana.

Bupeh ni mwimbaji wa Gopsel Hip Hop kutokea Nchini Kenya aliyekuwepo kuhudumu usiku wa jana alikuwa akifanya Gopsel Hip Hop iliyotokea kuwa baraka kwa idadi kubwa ya watu,pia akatoa ushuhuda wa maisha yake ambao uliweza kugusa maisha ya wengi.

Watu walipata kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yao. Night of worship ni Ibada itakayo kuwa katika mwendelezo wa Ijumaa usiku ya Kila mwezi ndani ya Kanisa la CCC Upanga.
VCC Praise and Worship Team kwa stage.
John Lisu

Backup Team ya John Lisu
Sarah katikati na wezenzake wakisupport John Lisu Team
Ilikuwa fullshangwe mpaka asubuhi Watu walipata mda wa kutosha kusifu na kuabudu
Glorious Celebration wakirecord Live ndani ya CCC Upanda usiku wa jana.
Paul na wenzake wa Glorious Celebration wakikamua vocal kwa stage.
Flora Mbasha na Mmewe pia walikuwepo kuwakilisha usiku wa jana.

Paul kwa stage na Umenifanya Ibada

Bupe kutoka Kenya kwa stage akifanya Gospel Hip Hop
Abella na Paula ni wadau walikuwepo katika Event hiyo usiku wa jana.
Bupe na Catheline wakifanya collabo ya Gospel Hip Hop
Video Production Crew wakifanya Live recording ya Glorious Celebration usiku wa jana
Chini ya Hackneel Video Production. 
Audio Production Crew wakiwa kazini kurecord Album ya Glorious Celebration usiku wa jana

Saturday, October 27, 2012

Yaliyojiri kwenye Mkesha maalumu wa Vijana @ St.Columbus

Pastor Deo Lubala
Pastor  Freddie Kyara
Word Alive Praise Team wakihudumu usiku wa jana St Columbus

  Jessica Honore na Team nzima  ya Word Alive Praise Team
Rose Mushi akifuatilia kwa makini

Rose Mushi akifundisha

Ilikuwa fullshangwe
Twende kazi....

Wednesday, October 24, 2012

JK ashauriwa na Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Kufuta Chaguzi Zenye Rushwa

Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Tanzania limemshauri  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete kutoa tamko la kufuta chaguzi zote zizogubikwa na rushwa ndani ya chama hicho ili kurejesha heshima kwa chama na serikali iliyopo madarakani. 

Tamko hilo limetolewa na Mchungaji wa kanisa hilo, William Mwamalanga, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kufuatia kauli ya Rais Kikwete kwamba vitendo vya rushwa vinavyojitoleza katika chaguzi za CCM vitakitumbukiza chama hicho kwenye shimo. 

Mwamalanga alisema rushwa ndani ya CCM  imekifanya chama hicho kukosa mwelekeo hivyo kinachotakiwa ni kwa Rais Kikwete kuchukua hatua ya kufuta matokeo yote ya viongozi waliochaguliwa kwa rushwa ili kurejesha heshima na imani kwa wananchi kwa chama hicho.

 “Rushwa ndani ya CCM imekuwa zaidi ya malaria, imekuwa zaidi ya ukimwi, kwa msingi huo kauli ya Rais kukemea rushwa haitoshi,maana tatizo hili ndani ya CCM  limebaki kama ngoma isiyokuwa na wachezaji,” alisema Mwamalanga.

Alisema CCM ndiyo chama tawala, hivyo Watanzania walitegema kuona kinakuwa chama cha mfano kupambana na rushwa badala yake kimekuwa kiongozi wa rushwa hali ambayo inazorotesha upatikanaji wa maendeleo nchini. 

Mwamalanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kurugenzi ya Kueneza Amani kwa Jamii  na dini zote nchini kama tatizo la rushwa litaachwa liendelee kushamiri ndani ya chama hicho kikongwe, itakuwa vigumu kukemea vyama vingine vya siasa iwapo vitachukua madaraka ya nchi. 

Alisema CCM ambayo ilitokana na Tanu ilijiwekea misingi mizuri ya kukataa rushwa, lakini hivi sasa kimekuwa chama kinachoongoza kwa rushwa. 

Kuhusu tatizo la kuchomwa kwa makanisa, alisema serikali inapaswa kuchunguza kwa umakini suala hilo kubaini chanzo na kwamba makanisa yote yaliyochomwa yajengwe kwa gharama za serikali. 

Rais  Kikwete akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), alitoa onyo kwamba vitendo vya rushwa vinavyojitokeza katika chaguzi za ndani za CCM visipodhibitiwa,  vitakitumbukiza chama hicho kwenye shimo. 

Malalamiko ya rushwa ndani ya chaguzi za CCM yametolewa na baadhi ya wagombea wa uenyekiti wa mikoa. Waliolalamika ni Clement Mabina (Mwanza), John Guninita (Dar es Salaam), Thomas Ngawaiya (Kilimanjaro), Makongoro Nyerere (Mara) na William Kusila (Dodoma).   

Thursday, October 18, 2012

MAOMBI NI NINI?

"Tufundishe Jinsi Ya Kuomba."

Je, umewahi kugundua kwamba wakati unapoamua kuomba unapata upinzani kutoka kwa ulimwengu, ukishirikiana na mwili wako, pamoja na Shetani? Unakuwa hutulii, unapata njaa, au usingizi, au unaanza kuwazia mambo mengine mengi unayolazimika kuyafanya.

1. Maombi Ni Nini?

Maombi ni mambo mengi kwa watu wengi. Ni mambo mengi kuanzia mazungumzo hadi kazi za mikono na za kiroho. Katika Lk 11:9,10 kuna ngazi tatu za maombi, nazo ni:

Ngazi Ya Kwanza Ni Rahisi Sana - Omba.
Omba – utakalo, ingawa Baba yako anajua hitaji lako hata kabla hujamwambia. Uwe kama watoto wadogo ambao ni mabingwa wa kuomba! Soma 2 Sam 5:17-25 ili uone namna Daudi alivyogundua jambo la kufanya kwa kumwuliza Mungu. Kufahamu mawazo ya Mungu kutakuongoza hatua kwa hatua kuelekea kwenye usalama mkuu (1 Yoh 3:21). Kwa upande mwingine soma kitabu cha Yoshua mlango wa 9 na hasa ule mstari wa 14 ili uone upumbavu wa kutokumwomba Bwana.

Ngazi Ya Pili Ni Nzuri Kwelikweli – Tafuta.

Kwa ufupi ni kumtafuta Yesu, kwa kuzingatia yeye ni nani. Furahia kutumia muda mrefu pamoja Naye, ukimwambia kila kitu, ukimsikiliza, bila kumletea mlolongo mrefu wa mahitaji.

Ngazi Ya Tatu Huubadilisha Ulimwengu – Bisha.

Bisha – mlangoni kwa mkuu wa Kanisa; nawe utamsikia Yesu akisema, “Ingia”. Anakualika wewe na waamini wengine kwenye maombi kwa sababu Yeye mwenyewe ni mwana maombezi, akiomba kwa ajili ya ulimwengu wa watu waliopotea. Kujiunga naye katika maombi kunaleta maombezi ya kwelikweli, yanayoweza kuchukua masaa au hata siku kadhaa (Ebr 7:24,25).

2. Ya Nini Kuomba?

Zipo sababu nyingi za kuomba, ambako ni mawasiliano ya njia mbili kati yako na Baba yako kadiri ukuavyo. Hata hivyo kulingana na ufahamu aliotupa Yesu katika Lk 11:21 tunazo sababu nzuri sana za kuomba:

    Yule mtu mwenye nguvu anamwakilisha Shetani.
    Nyumba yake ni dunia, na vitu vyake vinavyolindwa ni watu.
    Yule mwenye nguvu zaidi ni Yesu.
    Sisi tuko ndani yake na tumeketishwa pamoja naye (Efe 1:23) (Efe 2:6).
    Nyara ni watu wote wanaookolewa kupitia maombi; familia yako, jirani zako, na hata watu wengine walioko mbali.

3. Ni Nani Aombe?
Katika Lk 18:1, Yesu anawaambia wafuasi wake, waume kwa wake, wavulana kwa wasichana, vijana kwa wazee, kwamba wanapaswa kuomba kila wakati bila kukata tamaa. Maombi ni huduma yenye nguvu na iliyo wazi kwa kila mwamini, awe kijana au mzee.

4. Tuombe Tukiwa Wapi?

Katika nyakati za Biblia watu walisafiri ili wakafanyie maombi yao ndani ya Hekalu au katika maeneo mengine ya Kiyahudi ya kukusanyikia. Biblia inasema kwamba leo mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu, kwahiyo unaweza kuomba mahali po pote, wakati wo wote, na kwa namna yo yote: ukiwa umepiga magoti, ukiwa unatembea, ukiwa unafanya kazi, ukiwa umekaa, na hata ukiwa umelala chini.

5. Je, Tuombe Wakati Gani?
Yesu anasema tuombe  ‘kila mara,’ na Paulo anasema, ‘nyakati zote’. Iwe mchana au usiku, wakati wote kama nidhamu inavyodai, au kama moyo unavyoelekeza, tunaweza kuomba. Yesu anasema tuwe wavumilivu katika maombi, na Paulo anasema tuombe katika Roho kwa sala zote na maombi, ikiwa ni katika ukimya au katika msisimko mkubwa.

6. Je, Tuombe Namna Gani?

Katika Lk 11:2-4 Yesu alitufundisha namna ya kuomba. Haina maana kwamba turudie maneno hayo kila mara bila kufikiri au bila upendo kama ilivyo kwa baadhi ya makanisa, lakini ni lazima yaombwe kutoka moyoni na akilini pia.

Anza Kwa Kuzungumza Na Baba Yetu

Tukumbuke kwamba Baba yetu ni Baba aliye mkamilifu katika kutupenda na kututunza, si kama walivyo mababa wengi wa kidunia.

Litukuze Na Kulibariki Jina Lake

Chukua muda kumwabudu na kumshukuru kabla hujasema lo lote. Mwambie Mungu jinsi unavyompenda na umshukuru kwa upendo wake kwako, kwa familia yako, na kwa taifa lako (Yn 4:23).

Omba Kwamba Ufalme Wake Uje

Ufalme ni pale mfalme anakotawala,  kwahiyo mwombe Mungu kwamba Ufalme wake uje pale unakohitajika; katika maisha yako, katika familia yako, na katika taifa lako.

Omba Mapenzi Yake Yatimizwe

Kinyume na matukio maovu katika jamii.

Omba Mkate Wako Wa Kila Siku

Baba yuko radhi kutupatia mkate.

Mwombe Mungu Akusamehe Dhambi Zako

Acha damu ya Yesu itakase kila dhambi.

Na Kwa Kuwa Sasa Umesamehewa
Kusamehe wengine ndilo sharti la sisi kupokea msamaha wetu.

Uongozi Wa Mungu

Mwombe Mungu akuongoze maishani.

Mwombe Mungu Akuokoe Na Uovu

Uliojificha ndani yako, katika familia yako, na ndani ya vitu kama madawa ya kulevya na vita.

Mtukuze Kwa Ufalme Wake Na Utukufu

Hii ni fursa nyingine ya kuabudu, kusifu, na kutamka maneno ya imani. Ona jinsi muda unavyopita haraka unapoomba namna hii.

Hatimaye hapa pana siri ya maombi yenye nguvu. Yesu anahitimisha somo lake kuhusu maombi katika Lk 11:13 kwa kutuambia ni jinsi gani Baba alivyo radhi kutupatia Roho Mtakatifu. Kwahiyo kila mara mkaribishe Roho Mtakatifu aongoze  maombi, unapokuwa peke yako au kwenye kikundi, halafu uone jinsi atakavyokuwezesha kuomba vizuri. Masaa mengi yatapita kama dakika chache tu (Lk 11:5-8) (Efe 6:18).

 Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili

Tuesday, October 16, 2012

Kanisa lingine lateketezwa huko Kigoma

Muumini akishuhudia Kanisa la Pentekoste (MMPT) lililopo Buronge la Manispaa ya Kigoma/Ujiji, liliteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

Saa chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwasihi viongozi na waumini wa dini za Kikiristo na Kiislamu nchini kuwa wavulilivu na kujiepusha na vitendo vya kulipiza visasi, Kanisa la la Pentekoste (MMPT) lililopo Buronge katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji limechomwa moto na kutetekezwa kabisa na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku majira ya saa 4:00 usiku katika eneo la Buronge mjini Kigoma.

Kashai alisema kanisa hilo lilichomwa na watu wasiojulikana na kwamba mali mbalimbali zenye thamani ya Sh. 1,337,000 ziliteketea.

Alisema  sababu za kuchomwa kwa kanisa hilo hazijafahamika na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa huku upelelezi wa tukio hili ukiendelea ili kuwabaini wahalifu hao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

MCHUNGAJI ANENA

Mchungaji wa Kanisa hilo, Emmanuel Simon, alisema:

“Nilipata taarifa kuwa kanisa langu limeteketea kwa moto, nilikwenda Polisi Central kutoa taarifa ndipo tulikwenda eneo la tukio tukakuta kanisa lote limeteketea kwa moto.”

Alisema katika kanisa kulikuwa na mabechi 14, mlango mmoja, virago vitatu, masanduku ya sadaka na ubao wa kufundishia, vyote vikiwa na thamani ya Sh. 1,337,000.

Mchungaji Simon alisema hajui watu waliochoma kanisa hilo na kuiomba serikali iangalie matukio ya uchomaji wa makanisa yanayoendelea nchi nzima.

Pia, alilitaka Jeshi la Polisi kufanya doria kwenye makanisa wakati wa usiku ili kukomesha vitendo vya uchomaji wa makanisa.

Alisema kanisa ni taasisi ya jamii, hivyo anaomba serikali ichangie gharama ya ujenzi wa jengo hilo ili wananchi wanaoabudu katika kanisa hilo wapate sehemu ya kuabudia.

KANISA LA WAADVENTISTA LALAANI

Kanisa la Waadventista Wasabato limetoa tamko rasmi dhidi ya tukio la kuharibiwa kwa jengo la ibada la kanisa hilo lililoko Mbagala, jijini Dar es Salaam na kuchomwa moto kwa makanisa mengine ya Kikristo na watu wanaodaiwa kuwa ni waumini wa Kiislamu.

Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari mjini Morogoro jana, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Jimbo la Mashariki mwa Tanzania, Mark Malekana, alitaka serikali kulichukulia suala hilo kwa uzito wa kipekee.

Alisema licha ya kanisa hilo licha ya kupongeza kauli za viongozi wa madhehebu mengine ya dini na serikali za kukemea na kulaani viendo hivyo, lakini viongozi wa dini ya Kiislam nao wanapaswa kuwachukulia hatua za kinidhamu waumini wao wanaohatarisha amani .

“ Lazima hawa viongozi wa dini ya Kiislam wawachukulie hatua hao waumini ambao wameanza kuharibu amani ama sivyo jamii itakuwa na picha isiyo sahihi,” alisema.

Askofu huyo alisema matukio ya kushambulia na kuharibu majengo matakatifu ya ibada ya Kikristo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara na hata kusababisha wasiwasi kwa waumini wa dini hiyo, jambo ambalo likiachwa liendelee linaweza kuharibu amani nchini.

“Kanisa halikufurahishwa kabisa na kitendo cha mtoto kudhalilisha kitabu kitukufu cha Kuran na nailipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua zilizochukuliwa za kumuweka kituoni mtoto huyo kwa uchunguzi zaidi na kwa usalama,” alisema.

Aliongeza: “Kitendo cha kukamatwa na polisi kinaonyesha jinsi dola isivyochukulia kirahisi mambo yayoweza kuvuruga amani miongoni mwa jamii. Kwa kweli kitendo cha mtoto huyo ni cha aibu.”

Alisema kuwa bado kanisa lake linalaani vitendo vya watu wazima wenye kujua sheria za nchi, tena watu wa kiroho kuamua kuchukua hatua mkononi kwa kuvamia kituo cha polisi na kufanya uharibifu wa makanisa ambayo hata hayakuhusika na kitendo kilichofanywa na mtoto huyo.

“Kwa kweli vitendo hivyo havikupaswa kabisa kutendwa na watu wanaomcha Mungu, kwani mcha Mungu ni mtu anayetegemewa kuwa muhimili wa amani katika jamii na kutokana na hali hiyo, ninawaomba pia viongozi wa dini ya Kiislam wawachukulie hatua za kinidhamu hawa waumini wao wanaohatarisha amani yetu ama sivyo jamii itakuwa na picha mbaya isiyo sahihi,” alifafanua Askofu Malekana.

Askofu huyo alisema kuwa kanisa lake limefarijika kwa kauli zilizotolewa na viongozi mbalimbali akiwAmo Rais Kikwete; Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki; Kamanda wa Polisi Kanda na Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam kwamba zinazooneshwa kukerwa na matendo hayo na kuwataka waamini wa dhehebu hilo na Watanzania kwa ujumla kuwa wavumilivu wakati serikali ikishughulikia suala hilo.

Alisema Kanisa la Waadiventista Wasabato haliwezi kutafuta haki kwa kuvunja sheria, bali linapoona kuwa halitendewi inavyostahili, huitafuta haki kwa mujibu wa sheria.

Katika vurugu zilizotokea Oktoba 12, Mbagala jijini Dar es Salaam, jumla ya makanisa saba yalichomwa moto na mengine kuharibiwa na kikundi cha watu wanaotumia kivuli cha dini ya Kiislam kufanya vurugu hizo.

MBATIA: TUJADILI MUSTAKABALI

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  James Mbatia, amemuomba Rais Jakaya Kikwete kuwakutanisha viongozi wa dini  za Kikristo na Kiislam pamoja na wanasiasa ili kujadili namna ya kumaliza chuki  inayozuka kati ya dini hizo mbili.

Mbatia alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mstakabali wa vurugu zilizojitokeza wiki iliyopita huko Mbagala, baada ya kwa waumini wa Kiislam kuchoma makanisa kufuatia kijana mmoja wa anayedaiwa kuwa Mkristo kukojolea Kuran.

Mbatia alisema tukio hilo siyo jambo la kuchukulia kibusara eti kwamba lilisababishwa na watoto, bali kutafuta ufumbuzi wa chanzo cha matatizo hayo.

“Vitendo hivi havijaibuka jana wala juzi, tumeshuhudia mara kadhaa makanisa yakichomwa hata Zanzibar tumeshuhudia, hivyo watoto nao wanajifunza kutoka kwa wakubwa kwamba chuki ipo kati ya pande hizo, tusisubiri itokee kama nchi za wenzetu kwa sababu nao walianza hivi hivi,” alisema.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, aliongeza: “Tunaiomba serikali isifumbie macho jambo hili, bali ichukue jukumu la kuwakutanisha viongozi wa dini hizo pamoja na wanasiasa kuzungunguza kwa pamoja na kuangalia namna ya kumaliza chuki iliyopo hivi sasa.”

Alisema ni jambo la kushangaza kuona viongozi wa dini na wanasiasa wamenyamaza na pasipo kusema jambo lolote kuhusiana na vurugu zinazojitokeza.

“Ni jambo la kushangaza kuona kwamba hali inazidi kuwa tete, lakini wenye kuchukua maamuzi na kukemea wamekaa kimya, ni shetani gani ameingilia nchi hii au wana lao jambo?” alihoji.

Aidha, alisema baadhi ya wanasiasa nao wamekuwa ni kichocheo cha kujenga matabaka ya udini na kwamba kitendo hicho kinatakiwa kukemewa mara moja.

 126 KORTINI LEO

Watu 126 wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo jijini Dar es Salaam kufuatia vurugu zilizotokea katika eneo la Mbagala Kizuiani wiki iliyopita ambazo zilisababisha kuchoma moto makanisa na kuharibu mali.

Vurugu hizo zilisababishwa na kitendo mtoto wa miaka 14 kukojolea kurani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema jana kuwa askari polisi waliendelea na msako ili kubaini wahalifu katika tukio hilo, hata hivyo, alisema kuwa walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine sita juzi.

“Unajua jana asubuhi nilikuwa kwenye kikao kujadili suala hilo na kuamua kuwa muda wowote kuanzia leo (jana) watuhumiwa wote watakufikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria zitakamilika,” alisema Misime.

Watu hao wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani imedaiwa kuwa ni waumini wa dini ya Kiislam, waliovamia makanisa manne na kuyakuchoma moto, kwa madai kuwa mtoto mwenye umri wa miaka 14 alikojolea kitabu cha Kurani tukufu.

Kufuatia vurugu hizo, mali mbalimbali ziliharibiwa ikiwa ni pamoja vifaa vya kuendeshea ibada, vioo vya magari vilivunjwa, hasara kamili ya uharibifu huo haijafahamika.

Rais Kikwete katika hotuba yake juzi ya kuzima mbio za Mwenge wa uhuru na Kumbukumbu ya miaka 13 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliwataka viongozi wa dini hizo na waumini wao kuwa watulivu na wavumilivu wakati Jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi. Pia alisema wahusika wa vurugu hizo watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Waimbaji wa Injili waaswa kutoka kivingine

Mwimbaji Flora Mbasha

Pamoja na kuwepo wimbi kubwa la waimbaji wa muziki wa Injili, lakini bado hawajafikia hatua ya kubadilisha tabia za watu hususan vijana ambao wanakaa vijiweni kwa kujidunga sindano za Dawa za Kulevya.

Mbali na hilo waimbaji wametakiwa kutunga nyimbo ambazo zina mafundisho sahihi kwenye jamii, kwa lengo la kuhakikisha panakuwa na mabadiliko katika jamii hususani vijana wakaao vijiweni.

Si wengine bali ni wale waimbaji wa muziki wa Injili nchini, kwani wametakiwa kuimba nyimbo ambazo zina mafundisho ya kukemea na kufundisha jinsi ya kujiepusha na maambukizi ya ukimwi na matumizi ya dawa za kulevya.

Hayo yote yalitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Walk for Hope, Emmanuel Mbaule, alipokuwa akizungumza na waimbaji wa muziki wa Injili mjini hapa, jana.

Mbaule alisema kwamba Matamasha ambayo yanakusudiwa kufanywa na waimbaji wa nyimbo za Injili ni nyimbo ambazo zina ujumbe wa moja kwa moja wa kukemea maambukizi ya ukimwi na uvutaji wa dawa za kulevya.
Mwimbaji Rose Mhando

Upendo Nkone
Kwani tamasha hilo  linakusudia kuhakikisha waimbaji wanatumia muziki wao, kama sehemu ya kukuza uchumi badala ya kuimba nyimbo ambazo zinawanufaisha wengine.

Na inasikitisha kuona wapo baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili wanakuwa masikini bila kutambua kuwa nyimbo zao ni mali kubwa.

“Huwezi kuimba nyimbo za Injili na ukaendelea kuwa maskini, nyimbo za Injili ni muhimu sana, kwani unakomboa roho za watu na kuwafanya wapate neema ya ufalme wa Mungu na wala si vinginevyo.

Monday, October 15, 2012

Muumini akishuhudia Kanisa la Pentekoste (MMPT) lililopo Buronge la Manispaa ya Kigoma/Ujiji, liliteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

Saa chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwasihi viongozi na waumini wa dini za Kikiristo na Kiislamu nchini kuwa wavulilivu na kujiepusha na vitendo vya kulipiza visasi, Kanisa la la Pentekoste (MMPT) lililopo Buronge katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji limechomwa moto na kutetekezwa kabisa na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku majira ya saa 4:00 usiku katika eneo la Buronge mjini Kigoma.

Kashai alisema kanisa hilo lilichomwa na watu wasiojulikana na kwamba mali mbalimbali zenye thamani ya Sh. 1,337,000 ziliteketea.

Alisema  sababu za kuchomwa kwa kanisa hilo hazijafahamika na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa huku upelelezi wa tukio hili ukiendelea ili kuwabaini wahalifu hao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

MCHUNGAJI ANENA

Mchungaji wa Kanisa hilo, Emmanuel Simon, alisema:

“Nilipata taarifa kuwa kanisa langu limeteketea kwa moto, nilikwenda Polisi Central kutoa taarifa ndipo tulikwenda eneo la tukio tukakuta kanisa lote limeteketea kwa moto.”

Alisema katika kanisa kulikuwa na mabechi 14, mlango mmoja, virago vitatu, masanduku ya sadaka na ubao wa kufundishia, vyote vikiwa na thamani ya Sh. 1,337,000.

Mchungaji Simon alisema hajui watu waliochoma kanisa hilo na kuiomba serikali iangalie matukio ya uchomaji wa makanisa yanayoendelea nchi nzima.

Pia, alilitaka Jeshi la Polisi kufanya doria kwenye makanisa wakati wa usiku ili kukomesha vitendo vya uchomaji wa makanisa.

Alisema kanisa ni taasisi ya jamii, hivyo anaomba serikali ichangie gharama ya ujenzi wa jengo hilo ili wananchi wanaoabudu katika kanisa hilo wapate sehemu ya kuabudia.

KANISA LA WAADVENTISTA LALAANI

Kanisa la Waadventista Wasabato limetoa tamko rasmi dhidi ya tukio la kuharibiwa kwa jengo la ibada la kanisa hilo lililoko Mbagala, jijini Dar es Salaam na kuchomwa moto kwa makanisa mengine ya Kikristo na watu wanaodaiwa kuwa ni waumini wa Kiislamu.

Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari mjini Morogoro jana, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Jimbo la Mashariki mwa Tanzania, Mark Malekana, alitaka serikali kulichukulia suala hilo kwa uzito wa kipekee.

Alisema licha ya kanisa hilo licha ya kupongeza kauli za viongozi wa madhehebu mengine ya dini na serikali za kukemea na kulaani viendo hivyo, lakini viongozi wa dini ya Kiislam nao wanapaswa kuwachukulia hatua za kinidhamu waumini wao wanaohatarisha amani .

“ Lazima hawa viongozi wa dini ya Kiislam wawachukulie hatua hao waumini ambao wameanza kuharibu amani ama sivyo jamii itakuwa na picha isiyo sahihi,” alisema.

Askofu huyo alisema matukio ya kushambulia na kuharibu majengo matakatifu ya ibada ya Kikristo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara na hata kusababisha wasiwasi kwa waumini wa dini hiyo, jambo ambalo likiachwa liendelee linaweza kuharibu amani nchini.

“Kanisa halikufurahishwa kabisa na kitendo cha mtoto kudhalilisha kitabu kitukufu cha Kuran na nailipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua zilizochukuliwa za kumuweka kituoni mtoto huyo kwa uchunguzi zaidi na kwa usalama,” alisema.

Aliongeza: “Kitendo cha kukamatwa na polisi kinaonyesha jinsi dola isivyochukulia kirahisi mambo yayoweza kuvuruga amani miongoni mwa jamii. Kwa kweli kitendo cha mtoto huyo ni cha aibu.”

Alisema kuwa bado kanisa lake linalaani vitendo vya watu wazima wenye kujua sheria za nchi, tena watu wa kiroho kuamua kuchukua hatua mkononi kwa kuvamia kituo cha polisi na kufanya uharibifu wa makanisa ambayo hata hayakuhusika na kitendo kilichofanywa na mtoto huyo.

“Kwa kweli vitendo hivyo havikupaswa kabisa kutendwa na watu wanaomcha Mungu, kwani mcha Mungu ni mtu anayetegemewa kuwa muhimili wa amani katika jamii na kutokana na hali hiyo, ninawaomba pia viongozi wa dini ya Kiislam wawachukulie hatua za kinidhamu hawa waumini wao wanaohatarisha amani yetu ama sivyo jamii itakuwa na picha mbaya isiyo sahihi,” alifafanua Askofu Malekana.

Askofu huyo alisema kuwa kanisa lake limefarijika kwa kauli zilizotolewa na viongozi mbalimbali akiwAmo Rais Kikwete; Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki; Kamanda wa Polisi Kanda na Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam kwamba zinazooneshwa kukerwa na matendo hayo na kuwataka waamini wa dhehebu hilo na Watanzania kwa ujumla kuwa wavumilivu wakati serikali ikishughulikia suala hilo.

Alisema Kanisa la Waadiventista Wasabato haliwezi kutafuta haki kwa kuvunja sheria, bali linapoona kuwa halitendewi inavyostahili, huitafuta haki kwa mujibu wa sheria.

Katika vurugu zilizotokea Oktoba 12, Mbagala jijini Dar es Salaam, jumla ya makanisa saba yalichomwa moto na mengine kuharibiwa na kikundi cha watu wanaotumia kivuli cha dini ya Kiislam kufanya vurugu hizo.

MBATIA: TUJADILI MUSTAKABALI

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  James Mbatia, amemuomba Rais Jakaya Kikwete kuwakutanisha viongozi wa dini  za Kikristo na Kiislam pamoja na wanasiasa ili kujadili namna ya kumaliza chuki  inayozuka kati ya dini hizo mbili.

Mbatia alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mstakabali wa vurugu zilizojitokeza wiki iliyopita huko Mbagala, baada ya kwa waumini wa Kiislam kuchoma makanisa kufuatia kijana mmoja wa anayedaiwa kuwa Mkristo kukojolea Kuran.

Mbatia alisema tukio hilo siyo jambo la kuchukulia kibusara eti kwamba lilisababishwa na watoto, bali kutafuta ufumbuzi wa chanzo cha matatizo hayo.

“Vitendo hivi havijaibuka jana wala juzi, tumeshuhudia mara kadhaa makanisa yakichomwa hata Zanzibar tumeshuhudia, hivyo watoto nao wanajifunza kutoka kwa wakubwa kwamba chuki ipo kati ya pande hizo, tusisubiri itokee kama nchi za wenzetu kwa sababu nao walianza hivi hivi,” alisema.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, aliongeza: “Tunaiomba serikali isifumbie macho jambo hili, bali ichukue jukumu la kuwakutanisha viongozi wa dini hizo pamoja na wanasiasa kuzungunguza kwa pamoja na kuangalia namna ya kumaliza chuki iliyopo hivi sasa.”

Alisema ni jambo la kushangaza kuona viongozi wa dini na wanasiasa wamenyamaza na pasipo kusema jambo lolote kuhusiana na vurugu zinazojitokeza.

“Ni jambo la kushangaza kuona kwamba hali inazidi kuwa tete, lakini wenye kuchukua maamuzi na kukemea wamekaa kimya, ni shetani gani ameingilia nchi hii au wana lao jambo?” alihoji.

Aidha, alisema baadhi ya wanasiasa nao wamekuwa ni kichocheo cha kujenga matabaka ya udini na kwamba kitendo hicho kinatakiwa kukemewa mara moja.

 126 KORTINI LEO

Watu 126 wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo jijini Dar es Salaam kufuatia vurugu zilizotokea katika eneo la Mbagala Kizuiani wiki iliyopita ambazo zilisababisha kuchoma moto makanisa na kuharibu mali.

Vurugu hizo zilisababishwa na kitendo mtoto wa miaka 14 kukojolea kurani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema jana kuwa askari polisi waliendelea na msako ili kubaini wahalifu katika tukio hilo, hata hivyo, alisema kuwa walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine sita juzi.

“Unajua jana asubuhi nilikuwa kwenye kikao kujadili suala hilo na kuamua kuwa muda wowote kuanzia leo (jana) watuhumiwa wote watakufikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria zitakamilika,” alisema Misime.

Watu hao wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani imedaiwa kuwa ni waumini wa dini ya Kiislam, waliovamia makanisa manne na kuyakuchoma moto, kwa madai kuwa mtoto mwenye umri wa miaka 14 alikojolea kitabu cha Kurani tukufu.

Kufuatia vurugu hizo, mali mbalimbali ziliharibiwa ikiwa ni pamoja vifaa vya kuendeshea ibada, vioo vya magari vilivunjwa, hasara kamili ya uharibifu huo haijafahamika.

Rais Kikwete katika hotuba yake juzi ya kuzima mbio za Mwenge wa uhuru na Kumbukumbu ya miaka 13 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliwataka viongozi wa dini hizo na waumini wao kuwa watulivu na wavumilivu wakati Jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi. Pia alisema wahusika wa vurugu hizo watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Wednesday, October 3, 2012

Maaskofu Pentekoste waja juu dini kukashifiana

Maaskofu wa makanisa ya kipentekoste Mkoa wa Arusha  wameitaka serikali kuzuia baadhi ya madhehebu ya dini yanayokashifu dini nyingine  hadharani ili kuendeleza amani nchini.

Rai hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Maaskofu wa Makanisa hayo, Oral Sosi  muda mfupi baada ya kutawazwa kuwa Askofu mteule  wa Jimbo la Arusha wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God katika ibada iliyofanyika  Kanisa la Betheli Kijenge.

Sosi, alisema anashangaa serikali kukaa kimya wakati viongozi wa dini nyingine wakiwatukana wao na baadhi ya viongozi wa serikali.

“Kama kweli serikali ina nia ya dhati ya kuendeleza amani katika taifa letu wachukue hatua haraka kumaliza fedheha hii dhidi ya viongozi wetu na waumini wetu tunayofanyiwa na dhehebu lingine, ”alisema Sosi.

Alisema kwa muda mrefu viongozi wao wamekuwa wakitukanwa hadharani na hata kupitia chombo kimoja cha habari hali ambayo mara kadhaa iliamsha hasira kutoka kwa vijana wao..

“Natoa dukuduku langu kwa serikali itende haki kwa kila dhehebu haiwezekani dhehebu moja kuoekana linapendelewa hasa pale inapofanya mambo yanayohatarisha amani katika jamii, ”alisema Sosi.

Alisema hali hiyo inapaswa kudhibitiwa haraka ili kuendelea kuienzi amani iliyoasisiwa na viongozi waanzilishi wa Tanzania akiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Askofu huyo aliiihakikishia serikali kuwa kanisa hilo litaendelea kuwaelimisha waumini wake kutii sheria bila shuruti na kukemea vitendo vinavyokwenda kinyume na utu na maadili katika nchi.

Akitoa salamu za serikali katika ibada hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema serikali inaendelea kufuatilia suala hilo na kuonya kuwa itachukua hatua  dhidi ya mtu au kikundi chochote kitachoonekana kinatishai mshikamano na upendo katika jamii.

“Serikali yenu inalifahamu vyema tatizo hilo na inalifanyia kazi. Nawaomba kuwa wavumilivu hakuna mtu au kikundi chochote cha kidini kilichoko juu ya sheria ni lazima amani yetu tuilinde kwa nguvu zote, ”alisema Mulongo.

Tuesday, October 2, 2012

Semina Ya Vijana...'A Call To The Higher Dimension' Yaunguruma

Kanisa la Word Alive Sinza linaloongozwa na Askofu Deogratius Lubala lililoko Sinza Mori jijini Dar es salaam, limeandaa kongamano la kipekee la siku mbili litakalowahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali. Kwa mujibu wa waandaaji wa Kongamano hilo, kongamano hilo litafanyika jumamosi ijayo na jumapili (Tarehe6-7/10/2012) kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni ambapo chakula kitatolewa bure.Siku ya Jumapili kuanzia saa tisa mchana Kongamano litamalizika kwa IBADA KUBWA ya kusifu na kuabudu.

Kongamano hilo la vijana litakuwa likifanyika kila mwaka na kwa mwaka huu limebeba ujumbe usemao “CALL TO HIGHER DIMENSION”.Vikundi mbalimbali vya uimbaji vitahudumu vikiongozwa na Word Alive Praise Team.Kwa kijana yeyote ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam hii si ya kukosa ukizingatia waalimu watakaohudumu Mungu ameweka hazina kubwa ndani yao kwa utukufu wa wake.Lets meet Sinza Mori jumamosi na jumapili.

1.Rose Mushi
2.Pastor Isaack Mallonga
3.Pastor Daniel Musokwa
4.Lilian Modesta Mahiga
5.Pastor Deogratius Lubal 6.Ramsey Ngwelleja

Chuki ndani ya Kanisa huletwa na wenye fedha chafu

Askofu wa Kanisa la  Kianglikana nchini, Dk. Valentine Mokiwa,  amewataka watendaji wa kanisa hilo   kuwa macho na baadhi ya watu wenye uwezo mkubwa kifedha kupandikiza chuki  ndani ya madhehebu hayo.

Akizungumza  na waumini wa kanisa  hilo Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, mjini hapa wakati wa ibada ya shukrani  baada ya kumalizika kwa mgogoro  uliokuwa unaikumba kanisa hilo,  Dk. Mokiwa alisema imeibuka tabia kwa baadhi ya viongozi wa kanisa kuogopa  kuwakemea watu wenye uwezo  mkubwa kifedha  hata kama wanakiuka sheria za kanisa.

Aidha, kiongozi huyo  pia amewataka  watendaji  wa kanisa hilo kutokubali  kupokea fedha za muumini  yeyote zitakazobainika kuwa hazikupatikana kihalali. 

 “Ni vyema  kutafuta fedha kwa bidii ili kupambana na umaskini na sio dhambi mtu kuwa fedha nyingi lakini ni dhambi kutafuta fedha kwa njia zisizo halali na ni vibaya zaidi kutumia fedha hizo  kupandikiza chuki mahali popote  ikiwemo  ndani ya kanisa” alisema askofu  Mokiwa na kuongeza:

“Itakuwa dhambi kubwa kwa viongozi  wa madhehebu ya dini  kuwatetemekea  na kuwaweka mbele watu wenye fedha na kushindwa kuwakemea pale wanapokwenda kinyume  na kufanya hivyo ni kwenda kinyume  na maelekezo  ya kanisa na maelekezo  ya Mungu.”

 Askofu Mokiwa pia amewaonya waumini  wanaodhani kuwa kwa kutumia fedha zao  watapata nafasi  ya  kuyavuruga madhehebu ya dini na kuwataka viongozi wa madhehebu ya dini  kuwa macho na makundi  ya  watu   wa  aina hiyo ambayo  amedai yamekuwa yakiongezeka siku hadi  siku.

Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu  wa Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro  Stanele Hotay, pamoja na kuwashukuru waumini wa kanisa hilo kwa mshikamano walioonyesha wakati  wote wa mgogoro, aliwawataka kuendeleza msimamo huo.

Aidha, Askofu huyo  ameiomba serikali  kuendelea kushirikiana kwa karibu na viongozi  wa madhehebu ya dini katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kukabiliana na umaskini  unaoendelea kuikabili  jamii.

Wakiwasilisha salam za serikali, Mkuu   wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo  na Mkuu wa Mkoa  wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, walisema serikali  itaendelea kushirikiana na viongozi  wa madhehebu ya dini  na kuhakikisha  kuwa uhuru wa kuabudu  unadumishwa kwa mwananchi  wote.

Dk. Nchimbi  amewataka  waumini  wa madhehebu ya dini  wanaopambana na viongozi  wao  kuacha mara moja utaratibu huo  kwani  licha ya kuwa hauna tija utawasababishia kupata laana  toka kwa Mungu.

Monday, October 1, 2012

Padri akerwa viongozi kukumbatia rushwa, Awaasa waongoze kwa mfano wa Nyerere

Viongozi nchini wametakiwa kumuiga Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye aliongoza nchi kwa misingi ya Azimio la Arusha badala ya kukumbatia rushwa na ufisadi unaowanufaisha baadhi ya walioko madarakani.

Kadhalika, wametakiwa kuiga mfano wa Mwalimu Nyerere ambaye wakati wa uongozi wake, hakunyanyasa watu na alitaifisha hata shule zilizokuwa zinamilikiwa na Kanisa Katoliki ili watu wote wapate elimu sawa na kuwa wamoja bila kujali dini, itikadi, rangi wala kabila.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika la Farijika, Familia na Jamii Afrika Mashariki, Padre Baptiste Mapunda, wakati akiongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Manzese, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Farijika, Familia na Jamii Afrika Mashariki, Padre Baptiste Mapunda

Padri Mapunda alisema Nyerere, aliwaokoa Watanzania kutoka kwenye utumwa wa wakoloni na mabepari na alikuwa na unyeyekevu kama Musa alivyowaokoa Waisrael kutoka utumwani.

“Mwalimu Nyerere ni kama nabii, dunia nzima inaheshimu uongozi wake, alisisitiza watu wote kuepuka chuki na wivu na aliongoza kwa kutumia Azimio la Arusha, lakini sasa wajanja wachache wameliondoa azimio hilo na kukumbatia rushwa na ufisadi,” alisema katika mahubiri yake.

Aliongeza kuwa matajiri na mabepari wamevamia nchi kwa kujiita wawekezaji huku wazawa wakiishia kuwa maskini kwa sababu ya viongozi wachache wanaokula rushwa na kuangamiza walio wengi.

“Miaka 50 hakuna kilichofanyika zaidi ya kupoteza fedha huku wananchi wakililia huduma mbalimbali za kijamii. Kwa nini fedha hizo zisitolewe kwenye shule na hospitali ili watu waone serikali yao inawajali?,” Alihoji huku akishangiliwa na waumini waliohudhuria ibada hiyo.

Akizungumzia utoaji wa maoni kwenye mchakato wa Katiba mpya, Padri Mapunda, alisema kuna haja ya wananchi kupata Katiba mpya itakayoainisha matumizi ya rasilimali zilizopo nchini.

“Tunatakiwa kujua matumizi ya rasilimali zetu, maliasili, mikataba mibovu inayobomoa uchumi wa nchi yetu isifumbiwe macho vyote vianishwe kwenye Katiba mpya,” alisema na kuongeza:

“Wananchi wasiache kujitokeza kutoa maoni yao kwa kuwa hali sasa imekuwa siyo shwari hata uhuru wa habari hakuna, viongozi wachache wanakumbatia utumwa na kusahau uzalendo wao,” alisema.

Akifafanua zaidi, Padri Mapunda alisema maombi yanahitajika katika kipindi hiki cha kutoa maoni ya Katiba hiyo ili nchi ipate viongozi wanaojali bila kutanguliza fedha mbele na nchi irejee kama wakati wa hayati Mwalimu Nyerere.