Thursday, August 30, 2012

Mwanzo » Habari Askofu wa Jimbo la Mpanda afariki dunia

Enzi za Uhai wake
Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki  la Mpanda mkoani Katavi, Mhashamu Paschal William Kikoti (55), amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu huko katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Makamu wa Askofu wa Jimbo la Mpanda, Padri Patrick Kasomo, alitangaza msiba huo juzi usiku kwenye Kanisa Kuu la Jimbo la Mpanda muda kwa mamia ya wamumini waliokuwa wamekusanyika kanisani hapo.

Aliwaeleza waumini hao kuwa Askofu Kikoti  alipatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu Jumapili iliyopita saa moja asubuhi wakati akioga na ndipo alipoanguka ghafla akiwa bafuni kisha kupoteza fahamu.

Alisema baadaye alikutwa na mapadri na watawa walipokuwa wametoka kwenye katika ibada ya misa ya kwanza majira ya saa mbili na nusu asubuhi bila kuwa na fahamu.


Alisema Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) lilitafuta usafiri wa ndege siku hiyo kumsafirisha hadi Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza kwa ajili ya kupatiwa matibabu hadi juzi alipofariku dunia.

Baada ya Padri Kasomo kutowa taarifa hiyo, waumini wa kanisa hilo waliangua vilio na baadhi yao kupoteza fahamu.

Marehemu Askofu  Kikoti alizaliwa  katika Parokia ya Nyabula  mkoani Iringa mwaka  1957 na kupewa daraja la upadre Juni 29, mwaka 1988 mkoani humo.

Alipewa daraja la uaskofu Januari 14, 2001 iliyomfanya awe Askofu wa kwanza wa Jimbo jipya la Mpanda. Mwili wa Askofu Kikoti utawasili leo ukitokea Mwanza kwa wa ndege na anatarajiwaa kuzikwa Jumamosi ndani ya Kanisa Kuu la Mpanda.

MJENGO MPYA WA MHE. MCHUNGAJI GETRUDE RWAKATARE ULIOPO MBEZI BEACH DAR ES SALAAM..

Muonekano wa mbele wa hekalu la Mchungaji Rwakatare

MC Haris Kapiga wa Clouds FM akiwa na Mchungaji

Mc Harris Kapiga akiwa kazini.

 

Watu wakijiachia

Kabati la vyombo

Akiwa katika ofisi yake ya nyumbani, kuna sehemu ya kufanyia mikutano, Salon, Studio, na sehemu ya mazoezi.

Wakati wa msosi

Wadau wakijiachia kwenye moja wapo ya kochi  la kifahari mjengoni humo

Mambo ya dressing table

Mchungaji Getrude Rwakatare amehamia rasmi katika nyumba yake mpya iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam pembezoni mwa bahari ya Hindi. Inaripotiwa kuwa waumini wa kanisa lake wapatao 300 walifika mahali hapo kwa kushuhudia nyumba yake hiyo ya kifahari.

Kabla ya kuhamia kwenye hekalu lake jipya Mch. Mh. Getrude Pangalile Rwakatare alikuwa akiishi Mikocheni B katika nyumba nyingine ya kifahari pia.

Picha na Ruma Africa