Tuesday, October 16, 2012

Waimbaji wa Injili waaswa kutoka kivingine

Mwimbaji Flora Mbasha

Pamoja na kuwepo wimbi kubwa la waimbaji wa muziki wa Injili, lakini bado hawajafikia hatua ya kubadilisha tabia za watu hususan vijana ambao wanakaa vijiweni kwa kujidunga sindano za Dawa za Kulevya.

Mbali na hilo waimbaji wametakiwa kutunga nyimbo ambazo zina mafundisho sahihi kwenye jamii, kwa lengo la kuhakikisha panakuwa na mabadiliko katika jamii hususani vijana wakaao vijiweni.

Si wengine bali ni wale waimbaji wa muziki wa Injili nchini, kwani wametakiwa kuimba nyimbo ambazo zina mafundisho ya kukemea na kufundisha jinsi ya kujiepusha na maambukizi ya ukimwi na matumizi ya dawa za kulevya.

Hayo yote yalitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Walk for Hope, Emmanuel Mbaule, alipokuwa akizungumza na waimbaji wa muziki wa Injili mjini hapa, jana.

Mbaule alisema kwamba Matamasha ambayo yanakusudiwa kufanywa na waimbaji wa nyimbo za Injili ni nyimbo ambazo zina ujumbe wa moja kwa moja wa kukemea maambukizi ya ukimwi na uvutaji wa dawa za kulevya.
Mwimbaji Rose Mhando

Upendo Nkone
Kwani tamasha hilo  linakusudia kuhakikisha waimbaji wanatumia muziki wao, kama sehemu ya kukuza uchumi badala ya kuimba nyimbo ambazo zinawanufaisha wengine.

Na inasikitisha kuona wapo baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili wanakuwa masikini bila kutambua kuwa nyimbo zao ni mali kubwa.

“Huwezi kuimba nyimbo za Injili na ukaendelea kuwa maskini, nyimbo za Injili ni muhimu sana, kwani unakomboa roho za watu na kuwafanya wapate neema ya ufalme wa Mungu na wala si vinginevyo.

No comments:

Post a Comment