Friday, September 28, 2012

KONGAMANO LA WANAWAKE.....MWEZESHE MWANAMKE KIUCHUMI KWA MAENDELEO YA FAMILIA

Jukumu la mwanamke katika familia ni muhimu sana kwanza....Wanawake walio wengi wanatamani kuwa na kipato cha kutosheleza malengo yao na ya Kifamilia.

Ujasiriamali unawawezesha Wanawake kufanikiwa kiuchumi, huku wakiendesha Familia na kufanya shughuli zao kwa mafanikio makubwa zaidi.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Bethel, Sheila Mumy Bethel
Kwani Kongamano hili limeandaliwa na Wanawake waliofanikiwa kiuchumi na wenye nia ya kusaidia Wanawake wengine waweze kufanikiw akiuchumi na Malengo ni Wanawake wote wenye ndoto za mafanikio.

Na moja ya mambo ya kijamii unayoweza kufanya kama mwanamke , ni kujitambua wenyewe kwamba wewe ni nani, nini unamaanisha na wapi unataka kwenda?

Kongamano hilo litaendeshwa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Bethel, Sheila Mumy Bethel litakalowika ndani ya Hoteli ya Holiday Septemba 30 mwaka huu kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 12 jioni na kiingilio ni Shilingi elfu 10,000 tu...Ukiwa kama Mwanamke unayehitaji ndoto zako zitimie na hujui ufanye nini...basi usikose kwenda kwenye Kongamano hilo kwani hautaondoka kama ulivyoingia hali utaondoka ukiwa na kitu tofauti na ulivyokwenda.

Thursday, September 27, 2012

Pengo awataka wanawake kuchangia Katiba mpya

Askofu  Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp Kardinali Pengo, amewahimiza wanawake wakatoliki washiriki katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba yenye kukidhi matakwa ya Watanzania.

Akizungumza hayo juzi jijini Dar es salaam katika ufunguzi wa maonesho ya miaka 40 ya wanawake wa Katoliki Tanzania (Wawata) yaliyohusisha majimbo 34 ya kikatoliki nchini, alisema kutokana na changamoto wazipatazo wanawake hao katika shughuli zao za ujasiliamali, ni vyema wapewe elimu kuhusiana na ujasiliamali ili kupunguza tatizo la umaskini nchini.






“Dunia ya leo inahitaji sana upendo, imani na ushirikiano hivyo pandeni mbegu za upendo katika familia ili watoto waonje matunda ya mama na baba ili wakati wa kuandaa maonyesho mengine wazingatie malezi kwa watoto na vijana wao,” alisema Kardinali Pengo.

Pia, Pengo alisema mwanamke mkatoliki wa Tanzania anaelewa nafasi yake na wajibu wake wa kikristo kuanzia ngazi ya familia, jumuiya, kanisa, jamii na taifa kwa ujumla na kuwa na maendeleo ya kiuchumi ili kukidhi mahitaji ya familia.

Katibu Mkuu msaidizi wa Wawata Taifa, Sara Kessy, alisema changamoto zinazowakabili ni pamoja na wengi wao kutokuwa na elimu ya biashara, ubunifu na uzoefu, hali inayopelekea kuona ugumu wa kuendesha biashara zao.

Maonesho hayo yaliyohudhuriwa na wageni kutoka nchi mbalimbali pamoja na Balozi wa Baba Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu Francisco Padella.

SOUL BREAKFAST SEASON II EPISODE IX

Kwa nini uwe ni mtu wa kuhadithiwa kila mara? Ni baada ya mwezi mmoja kupita Program ya Wanafunzi wa rika zote pamoja na wadau mbalimbali hapa mjini hujulikana kama SOUL BREAKFAST iliyokuwa ikiongozwa na Kijana mwenye vipaji lukuki si mwingine bali ni Samuel Sasali 'Papaa Ze Blogger' aliyatawala madhabahu na Mada ya THINK DIFFERENTLY ,MAKE A DIFFERENCE.

Septemba 29 mwaka huu, mishale  ya saa 8:30 Asubuhi kutafungua uku wa Season II Episode IX ndani ya Kanisa la  VICTORIA CHRISTIAN CENTER wengi hupenda kutumia kifupisho cha VCC...lililopo eneo la Victoria Petrol Station.

Safari hii madhabahu yanakwenda kutawaliwa na mwongozaji mwingine machachari ambaye ni Director of Women Ministry Mrs Florence Mbago atakuja na mada isemayo ENJOYING YOUTHOOD IN CHRIST.

Tuesday, September 25, 2012

Unahabari kwamba Sigara, pombe hatari kwa afya yako?

Tafiti za kisayansi zinazofanywa duniani kote zimeonyesha kuwa uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe, ni chanzo cha magonjwa mengi kwa binadamu ikiwa ni pamoja na saratani na magonjwa ya moyo.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Marina Njelekela aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwenye ufunguzi wa semina ya siku 10, ya programu maalumu ya mafunzo kwa madaktari na wauguzi wanaotibu magonjwa ya moyo na saratani ya matiti.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Marina Njelekela


Alisema baadhi ya vyakula na vidonda vya tumbo ni vitu ambavyo vinasababisha saratani kwa kasi zaidi pamoja na magonjwa ya moyo, pia alitoa wito kwa Watanzania waache pombe na sigara ili kupunguza idadi ya watu wengi wanaokufa kwa saratani kila mwaka.

Programu hiyo ni mpango wa pamoja kati ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili (Muhas), Hospitali ya Saratani Ocean Road na Germany Foundation, lengo lake likiwa ni ufunguzi wa kitengo cha mafunzo kinachohusiana na magonjwa ya saratani na tumbo, elimu na mafunzo kwa wauguzi na madaktari.

Katika semina hiyo, kutakuwepo na mafunzo ya vitendo ambapo Ujerumani imetoa vifaa vyenye thamani ya Sh. Milioni 7.5 na pia wanafunzi wanne kutoka Muhas ambao nao watakuwa kwenye mafunzo  hayo yanayohusisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Naye Kaimu Mkuu wa kitengo cha mafunzo ya kitengo cha tiba na magonjwa ya mfumo wa chakula Dk. John Rwegesha, alisema magonjwa yasiyoambukizi kama Malaria, kisukari, saratani, figo yanashika kasi hivyo wauguzi wanatakiwa wapewe mafunzo ya magonjwa hayo.

Profesa Rudolf Arnold kutoka Chuo Kikuu cha Ujerumani, alisema  amefurahi kuanzishwa kwa programu hiyo,  ambayo itasaidia wananchi wa EAC kwa ujumla.

Sarakasi Mama Afrika kuunguruma Alhamisi


Utambulisho wa maonesho ya sarakasi ya Mama Afrika yatakayoanza Alhamisi na kumalika Oktoba 4 ulifana jana wakati ulipofanyika kwenye ukumbi wa Mancom Centre New World Cinema uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya huduma za simu ya Tigo, yana lengo la kukuza sanaa na utamaduni wa Mtanzania. 



Akizungumza na waandisho wa habari wakati wa uzinduzi wa maonesho hayo jana, Mkurugenzi wa Mancom Centre, Constantine Magavilla, alisema kuwa maonesho ya mwaka huu yatapambwa na nyimbo za kitamaduni na za muziki wa kizazi kipya, mazingaombwe na michezo mbalimbali.



“Tunajivunia sana mafanikio ya maonesho ya Mama Afrika kwa miaka yote. Tunawashukuru Tigo kwa mchango wao mkubwa katika maonesho haya,” alisema Magavilla.


Afisa Uhusiano wa Tigo, Alice Maro alisema kuwa kampuni yao inajivunia mafanikio ya maonesho hayo kitaifa na kimataifa na kwamba wataendelea kuyapa kipaumbele ili kukuza sanaa na utamaduni wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Moja ya Sarakasi itakayorindima ndani ya Mama Afrika

Hapo jinsi itakavyokuwa siku hiyo
Maonesho ya Mama Afrika yalianzishwa mwaka 2003 kama shule ndogo ya sarakasi na Winston Ruddle aliyekuwa mkurugenzi na mwanzilishi.



Aflewo Nairobi Ni Next Level.

Tamasha la Kusifu na Kuabudu  Africa Lets Worship (AFLEWO) linalojumumisha baadhi ya Nchi za Afrika mwanzo wa weekend hii yaani siku a Ijumaa katika Jiji  la Nairobi nchini Kenya lilifanyika na kuhudhuriwa na Idadi kubwa ya watu katika kumsifu na kumtukuza Mungu.

Baadhi ya vikundi mbalimbali vya uimbaji vilikuwepo kuhudumu katika Tamasha hilo,bila kusahu Wachungaji mbalimbali kutoka nchi jirani katika kuwakilishi katika Tamasha hilo lisilo kuwa na tofauti za kidini wala kikabila bali kwa lengo la kuinua Sifa mbele za Mungu na kuomba kwa ajili ya Bara la Africa na Viongozi wake.

Miezi kadhaa iliyopita lilifanyika Dar-es-Salaam Tanzania,na baadaye kufanyika sehemu mbalimbali za Nchi na majiji mbalimbali Barani Africa ikiwa ni kwa lengo la Kuunganisha watu kwa nia ya Kusifu na Kuabudu Nchi hadi Nchi na Mwaka hadi Mwaka.


The Voice Wakienda Sawa.
Ilikuwa full anointing watu wakideep katika maombi

Bass Guitar in Action Aflewo  2012

Aflewo Praise and Worship Team 2012


Pastor Safari kutoka DPC Dar es salaam Tanzania, akitoa Neno Aflewo Nairobi 2012

Ilikuwa Fullshangwe

Africa Lets Worship (Aflewo ) Nairobi 2012

 Sehemu Ya Umati Wa Watu Waliohudhuria Aflewo Nairobi.

 Praise Team Ya Tanzania Wakiwa Jukwaani.


Ni Wakati Sasa wa Watanzania Ku Support Events zetu hasa Makampuni Ya Kikristo.

 Watu wakipokea anointing

Hapo kazi ilipamba moto

 Bila Shaka Ayalikuwa mambo yetu Yaleeeeee

Wazee Wa Kazi The Voice From Tanzania Wakifanya mambo Jukwaani.

Watu Wakiwafurahia The Voice Jukwaani.

Aflewo Team Kutoka Tanzania Ikiwa Jukwaani

 Mwenyekiti wa Aflewo Tanzania Geofrey Obiero akiwa ndani ya Aflewo Nairobi

 Hii nahisi Ilikuwa Ruka Kimasai....John Kagaruki akiwa hewani na Pastor Safari Wakati wa Kuongoza Praise Ndani Ya Aflewo Nairobi.

Tuesday, September 18, 2012

NDOA NI NINI?

                    MAANA HALISI YA NDOA NI IPI?


Ni  Muungano wa Mwanaume na Mwanamke unaokubalika kiutamaduni na Kidini ambao na unatarajiwa kudumu, kuwapa haki sawa za kijinsia na kutosheleza majukumu mengine ya kijamii.

Mbali na hilo watu wengi watu wengi siku hizi wamekuwa wakiishi maisha ya ndoa kama fasheni hali ambayo imekuwa ikishusha hadhi ya ndoa, na si jambo la ajabu kusikia ndoa iliyofungwa wiki moja iliyopita imevunjika baada ya wanandani hao kutwangana makonde na kusambaratika.

UNAFAHAMU KWAMBA KATIKA NDOA KUNA MATABAKA MAKUU MAWILI?

Tabaka lwa kwanza ni kwa wanandoa kufurahia Ndoa yao na tabaka la pili ni la wanandoa kuijutia ndoa yao, hakika ndoa inaraha sana na nitendo la heshima mbele za Mungu.

Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini siku ya Harusi wanandoa wote huwa na furaha? Na Je? furaha hiyo baadaye hupotelea wapi? Hakuna mwanandoa yeyote ambaye huwaza kama siku moja yeye na mwenzi wake wanaweza kukorofishana na kutukanana matuzi mazito ambayo hugeuka kuwa sumu ndani ya ndoa yao.
                                    
Siku ya harusi kila mmoja huisubiri kwa shauku kubwa na kuona siku kama haziendi ili wanandoa hao wawe pamoja kwenye jahazi la ndoa ya maisha. Baada ya muda  mambo hubadilika kwa baadhi ya wanandoa pindi wanapoanza maisha ya pamoja.

Kabla sijaendelea naomba kukuuliza wewe uliyendani ya NDOA...Je ulishawahi kujiuliza ni kwanini furaha mliyokuwa nayo wakati hamjaoana leo hii haipo tena? Kumbuka mara nyingi penzi linalotolewa wakati wa uchumba huwa lina mbinu nyingi za kusomana tabia na kila mmoja hupenda kuficha tambia yake mbaya aliyonayo.

Ni suala gumu kigodo kwa wanandoa ambao kila mmoja amekulia kwenye  malezi tofauti kukaa na kujenga tabia moja. Wakati watu wanapokuwa katika hatua ya uchumba hushindwa kusomana vizuri tabia zao ni kutokana na umbali walionao.

Kwa sababu kila mmoja anakuwa kwao ama kwake hali ambayo hutoa muda mwingi wa kumkumbuka mpenzi wake.( Ama hakika ndoa ni furaha, Kabla ya kutamka maneno ya ahadi mbele ya mashahidi kanisani huku taaaratibu wakivishana Pete ya Ndoa mme wake mpendwa fulani tayari kwa kuanza safari ya maisha ya ndoa yeye raha teeeeele!) Kipindi hicho wachumba hao hutumiana ujumbe mfupi kupitia mitandao kama Simu ama Email ili kila mmoja kuonyesha ni kwa jinsi gani anampenda mwanandani wake mtarajiwa.

Wahusika hao hujitahidi kutumiana maneno mazuri na yenye kuvutia hisia ya mahaba hali ambayo uzidi kuongeza upendo kwa pande zote mbili, na maneno hayo huongeza shauku kwa walengwa hao kuwa na shauku ya kuwa pamoja wakidhani kuwa siku zote mambo yatakuwa hivyo.

Kwa kipindi hicho wachumba hao huwa wanaelewana kwa kila jambo wanalopenda lifanyike na furaha ya Uchumba huo kama nilivyosema hapo awali hunogeshwa na umbali uliopo kati ya wahusika hao.

Wakati mwingi mmoja wapo anapotakiwa na mwenzake wakutane sehumu wanayoona inafaa kwa ajili ya mazungumzo yao ya faragha, na  hulazimika kuwadanganya wazazi wao ama ndugu zao wanaoishi nao kwamba wanaenda kwa jamaa zao na atachelewa kurudi.
                                        
Pindi mazungumzo yao yanapoanza huku muda ukizidi kwenda wachumba hao hutamani muda urudi nyuma ili waendelee kuongea na kupeana habari za hapa na pale kuhusu maisha yao ya badae, sasa shauku hiyo ya kuwa pamoja hupotelea wapi baada ya kuoana ambapo huwa kuna muda mrefu wa kuwa pamoja tofauti na kipindi kile walipokuwa wanaona muda unaenda na mazungumzo yao bado yanaendelea?

Nadhani utaungana na mimi kwamba kwa baadhi ya wanandoa mambo hayo hupotea pindi wanapoingia ndani ya ndoa kutokana na muda mwingi kuwa pamoja, na utakuta wanaongea mambo yao mpaka yanaisha.

Siku zote mwanadamu hakosi kuwa na madhaifu maishani mwake, kipindi hicho wanandoa hujikuta wapo kwenye wakati Mgumu pindi mmoja wapo anapofanya kosa hata si kwa makusudi.

Na inawezekana akawa ni mama kawa mkorofi ama baba ama wote kwa pamoja, na hiyo humfanya kila mmoja kujiona anahaki ya kufanya atakavyo na hayupo tayari kukosolewa.

Ni imani yangu kuwa kila mwanandoa siku ya kufunga ndoa huwa kunaviapo ambavyo hutamkwa na wahusika wote, kwamba  watakuwa tayari kuishi kwenye maisha ya raha na shida, iwe magonjwa nk. Lakini mambo huwa sivyo pindi safari ya maisha ya NDOA inapoanza.

SUMU YA MAISHA YA NDOA

Hakuna asiyefahamu kwamba asilimia kubwa ya vitu tunavyovitumia vina sumu, na hatuoni madhara ya sumu hiyo kutokana na kufuata taratibu za matumizi na vitu tunavyovitumia. Kwa Mfano mzuri ni dawa ya panado ambayo mtu anapoumwa kichwa hutumia dawa hiyo ili kuondoa maumivu hayo, na dawa hiyo huwa haitoi madhara yoyote. Lakini dawa hiyo ukinywa kinyume na masharti yake lazima madhara uyapate kama si kufa tambua utaugua zaidi.

Mambo hao kwanza kabisa ni heshima, upendo wa dhati, mawasiliano mazuri katika familia, kusaidiana na Uvumilivu. Haya ni mambo muhimu sana kwa wanandoa.

Kumbuka kwamba wanandoa wanaokosa mambo kama Heshima, Upendo wa dhati, Mawasiliano mazuri kwenye familia  ndoa yao lazima iwe mashakani na ugomvi hauwezi kuisha kamwe. Kwa wanandoa upendo unapotawala ndani ya nyumba huifanya ndoa hiyo kuchanua kila mara na hiyo huambatana na uvumilivu.

Neno jingine ambalo wengi huliona kama halina maana ni SAMAHANI... pindi mmoja wenu anapokosea, inapotokea ukamkosea mwenzako jitahidi kuomba samahani badala ya kukaa kimya na ukifanya hivyo itaonekana unadharahu ana kiburi.

Ukiyazingatia hayo yote ni lazima ndoa yako iwe na furaha siku zote. Kwa leo niishie hapa baada ya hapa nitakulete sababu za mwanamke kwenda nje ya ndoa, na kisha mwanaume naye kwenda nje ya ndoa. Nakaribisha maoni na ushauri juu ya yale uliyoyasoma hapo juu. Pia na wewe unaruhusiwa kutoa somo ama kufundisha jambo lolote ulilonalo kwa ajili ya faida ya sisi tusiojua....Je Sababu hizo za wanandoa kutoka nje ya Ndoa wazijua ni zipi?....Ambatana nami wiki ijayo siku kama ya leo.

MATUKIO MBALIMBALI YALIOJIRI KWENYE SEMINA ILIYOENDESHWA NA REV. ADAM HAJJ NDANI YA VCCT KWA SIKU 8

Pastor Joyce Nkone

Rev. Adam Hajj akitoa mafundisho



"Asante Yesu kwa Wema wako"....Rev Dr. Huruma Nkone


Happy na tabasamu lenye ukuu na mwenzake

Mpendwa Naomi na mwenzake nao walikuwepo hapo ni kabla ya semina kuanza

Kaka Misana Manyama akimsifu Mungu na watumishi wenzake


Wapendwa wakimsifu Mungu

Rev. Dr. Huruma Nkone akimsifu Mungu

Sifa za Yesu zivume


Wapendwa wakimtukuza Mungu

Ni kwa utukufu wa Bwana

Safi

Mungu ni mwema

Watoto nao hawakuwa nyuma walimsifu na kumtukuza Mungu kwa kucheza pia

Add caption

Elisha akimtukuza Mungu na wapendwa wengine

Sifa kwa Bwana

Johnson akiwaongoza wenzake katika kusifu na kuabudu


Rev. Dr. Huruma Nkone akimsifu Mungu

Upendo Nkon

Rev. Adam Hajj na mkewe wakiteta na mtoto


Upendo Nkon akimtambulisha Johnson kwamba ni mmoja kati ya washiriki walioshiriki kweny albamu yake

Johnson na Mwimbaji wa nyimbo za kumsifu Mungu Upendo Nkon

Upendo wa Yeu ukitawala


Daniel na Fredy



Wapendwa katka Bwana wakisifu na kuabudu














baba na mwana

Kulikoni?...kila mmoja alikuwa busy

Fredy na Christina

Fredy na Daniel baada ya ibada ya pili kuisha jumapili

Tabasamu lilitawala kila mahali siku hiyo

Daniel na Jackie

Ni kwa Neema ya Bwana


Papaa Ze Blogger akiwa na Fredy

Rev. Dr. Huruma Nkone akiwa mazabahuni



Rev. Adam Hajji na mkewe

Dada Miriam Lukindo akiserebuka







Tabasamu lenye utukufu wa Bwana lilitawala kwa wapendwa




Hapo wapendwa wakingoja kupewa baraka za mwisho siku ya mwisho ya semina