Thursday, August 30, 2012

Mwanzo » Habari Askofu wa Jimbo la Mpanda afariki dunia

Enzi za Uhai wake
Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki  la Mpanda mkoani Katavi, Mhashamu Paschal William Kikoti (55), amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu huko katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Makamu wa Askofu wa Jimbo la Mpanda, Padri Patrick Kasomo, alitangaza msiba huo juzi usiku kwenye Kanisa Kuu la Jimbo la Mpanda muda kwa mamia ya wamumini waliokuwa wamekusanyika kanisani hapo.

Aliwaeleza waumini hao kuwa Askofu Kikoti  alipatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu Jumapili iliyopita saa moja asubuhi wakati akioga na ndipo alipoanguka ghafla akiwa bafuni kisha kupoteza fahamu.

Alisema baadaye alikutwa na mapadri na watawa walipokuwa wametoka kwenye katika ibada ya misa ya kwanza majira ya saa mbili na nusu asubuhi bila kuwa na fahamu.


Alisema Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) lilitafuta usafiri wa ndege siku hiyo kumsafirisha hadi Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza kwa ajili ya kupatiwa matibabu hadi juzi alipofariku dunia.

Baada ya Padri Kasomo kutowa taarifa hiyo, waumini wa kanisa hilo waliangua vilio na baadhi yao kupoteza fahamu.

Marehemu Askofu  Kikoti alizaliwa  katika Parokia ya Nyabula  mkoani Iringa mwaka  1957 na kupewa daraja la upadre Juni 29, mwaka 1988 mkoani humo.

Alipewa daraja la uaskofu Januari 14, 2001 iliyomfanya awe Askofu wa kwanza wa Jimbo jipya la Mpanda. Mwili wa Askofu Kikoti utawasili leo ukitokea Mwanza kwa wa ndege na anatarajiwaa kuzikwa Jumamosi ndani ya Kanisa Kuu la Mpanda.

No comments:

Post a Comment