Tuesday, September 25, 2012

Sarakasi Mama Afrika kuunguruma Alhamisi


Utambulisho wa maonesho ya sarakasi ya Mama Afrika yatakayoanza Alhamisi na kumalika Oktoba 4 ulifana jana wakati ulipofanyika kwenye ukumbi wa Mancom Centre New World Cinema uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya huduma za simu ya Tigo, yana lengo la kukuza sanaa na utamaduni wa Mtanzania. 



Akizungumza na waandisho wa habari wakati wa uzinduzi wa maonesho hayo jana, Mkurugenzi wa Mancom Centre, Constantine Magavilla, alisema kuwa maonesho ya mwaka huu yatapambwa na nyimbo za kitamaduni na za muziki wa kizazi kipya, mazingaombwe na michezo mbalimbali.



“Tunajivunia sana mafanikio ya maonesho ya Mama Afrika kwa miaka yote. Tunawashukuru Tigo kwa mchango wao mkubwa katika maonesho haya,” alisema Magavilla.


Afisa Uhusiano wa Tigo, Alice Maro alisema kuwa kampuni yao inajivunia mafanikio ya maonesho hayo kitaifa na kimataifa na kwamba wataendelea kuyapa kipaumbele ili kukuza sanaa na utamaduni wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Moja ya Sarakasi itakayorindima ndani ya Mama Afrika

Hapo jinsi itakavyokuwa siku hiyo
Maonesho ya Mama Afrika yalianzishwa mwaka 2003 kama shule ndogo ya sarakasi na Winston Ruddle aliyekuwa mkurugenzi na mwanzilishi.



No comments:

Post a Comment